LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ibada ya leo "Mwili na Viungo vyake"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Karibu kwenye ibada hii kutoka Kanisa la KKT Usharika wa Kijitonyama Jijini Dar es salaam Dar es salaa. SOMO: MWILI NA VIUNGO VYAKE (Kupata ushindi dhidi ya upinzani wa mwili) "Pua na Mdomo" Mwanzo 2 : 7 Zaburi 19 : 14, 141 : 3 Isaya 11 : 4 1 Wakorintho 12 : 20 -23 . Mwanzo 2 : 7 7

Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Zaburi: 19: 14 14 Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. Zaburi 141: 3 3 Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu. 

Isaya 11: 4 4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. 1 Wakorintho 12 : 20 - 23 20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. 

21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. 22 Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. 23 Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. 
Mhubiri: Mwl : Emanuel Shemdoe
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.