LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya MISA Tanzania yatoa mafunzo kwa wanahabari Kanda ya Ziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Internews imeandaa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Mwanza ili kuwajengea uwezo kuhusu sheria mpya za vyombo vya habari na haki ya upatikanaji taarifa. 

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia leo Februari 16, 2019 yanafanyika Bariadi mkoani Simiyu ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini Tanzania ambayo yamekuwa yakitolewa na MISA Tanzania.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkufunzi wa mafunzo hayo, Sengiyumva Gasirigwa (kulia) akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika utetezi wa haki za binadamu.
Mafunzo hayo yanagusia sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016, Sheria ya Taifa ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma za Mitandao ya Kijamii ya mwaka 2015 pamoja na Kanuni zake.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Clonel Mwegendao (kulia) kutoka SACHITA FM iliyopo Tarime mkoani Mara akieleza matarajio yake ambapo amesema anatarajia kutambua sheria mpya za habari, changamoto zake na namna ya kukabiliana nazo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Edna Elisha (kulia) kutoka Jembe FM ya Jijini Mwanza amesema mafunzo hayo yatamjengea uelewa mpana kuhusu sheria ya huduma za habari na hivyo kutimiza vyema majukumu yake.
Mshiriki wa mafunzo, Hellen Mtereko kutoka City FM Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki Raphael Okelo wa Gazeti Majira kutoka Bunda mkoani Mara akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Dinna Maningo akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Derick Milton wa Gazeti Mtanzania mkoani Simiyu akieleza matarajio yake baada ya mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Machunda Nicholaus wa Sibuka FM mkoani Simiyu akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Hassan Ramadhan wa Star TV Jijini Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Neema Evance wa Azam TV mkoani Simiyu amesema sheria yoyote mpya inakuja na changamoto zake hivyo mafunzo hayo yatamjengea uwezo kutambua sheria mbalimbali za vyombo vya habari na namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Washiriki wa mafunzo hayo.
Afisa Utawala na Fedha kutoka taasisi ya MISA Tanzania, Andrew Marawiti (kushoto) akiteta jambo na Afisa Habari na Utafiti wa taasisi hiyo, Neema Kasabuliro (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.