LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ratiba ya ziara ya Makamu wa Rais mkoani Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mamia ya wakazi wa Mkoa Shinyanga wamejitokeza kumlaki Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan anayeanza ziara ya kikazi mkoani humo, hii leo February 26, 2019.

Mama Samia amepokelewa katika Kata ya Tinde, Halmashauri ya Wilaya Shinyanga akitokea mkoani Tabora alikohitimisha ziara yake ya kikazi kuanzia Februari 22, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wakazi wa Mkoa Shinyanga katika eneo la Tinde akitokea mkoani Tabora.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Bi. Zainab Telack (kushoto), Februari 26, 2019 Mama Samia atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Shinyanga, Februari 27, 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Februari 28, 2019 Halmashauri ya Wilaya Kishapu, Machi Mosi, 2019 Halmashauri ya Wilaya Msalala na Kahama Mji, Machi 02,2019 Halmashauri za Wilaya Msalala na Ushetu na Machi 03, 2019 hitimisho la ziara hiyo kwa kufanya majumuisho.
Sehemu ya wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kumlaki Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan katika Kata ya Tinde.
Sehemu ya wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kumlaki Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan katika Kata ya Tinde.
Mapokezi ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan mkoani Shinyanga.
Shinyanga

No comments:

Powered by Blogger.