LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makamu wa Rais awachana Tabora “tunasikia lele lele, pepe pepe”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi kupita mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chipukizi, Manispaa ya Tabora ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.

Kabla ya mkutano huo, Mama Samia alikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Maili Tano Ipuli kilichopokea shilingi milioni 400 kutoka serikalini kutekeleza ujenzi huo kupitia mfumo wa “Force Account” na baadae kufungua na kuongoza kongamano la wadau wa mazingira mkoani Tabora.

Ziara ya Makamu wa Rais, Mama Samia mkoani Tabora ilianza Februari 22, 2019 na imetamatika hii leo Februari 26, 2019 kwa kufanya majumuisho ya ziara hiyo kwa kukutana na viongozi pamoja na watendaji mbalimbali mkoani Tabora kabla ya kuelekea mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ya siku sita hadi Machi 03, 2019 mkoani humo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan alikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Maili Tano Ipuli Manispaa ya Tabora.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan alikabidhi vyetu vya shukrani kwa wadau wa mazingira kwenye kongamano la wadau wa mazingira mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri (kulia), akifurahia jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba akiwasilisha salamu za wizara hiyo kwenye kongamano la wadau wa mazingira mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri (kushoto), akizungumza kwenye kongamano la wadau wa mazingira mkoani humo.
Wadu mbalimbali wa mazingira wakiwa kwenye kongamano hilo.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan alizindua mnara huu wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira mkoani Tabora.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na vingoni mbalimbali na wanafunzi mkoani Tabora baada ya kuzindua mnara wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira mkoani Tabora.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.