LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makamu wa Rais akabidhi hundi ya milioni 40 kwa wanawake na vijana wilayani Sikonge

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Makamu Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan leo amekabidhi hundi ya shilingi milioni 40 kwa ajili ya vikundi 11 vya wanawake na vijana, iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya Sikonge mkoani Tabora kutokana na makusanyo ya ndani.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa takwa la kisheria kwamba asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri zote nchini, sharti itolewe kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kiuchumi.

Mama Samia anaendelea na ziara yake ya siku tano mkoani Tabora aliyoianza Februari 21, 2019 ambapo hii leo amekagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Sikonge pamoja na kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa TASAF.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.