LIVE STREAM ADS

Header Ads

"Tunapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli” DC Ikungi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu akizungumza na BMG kando ya warsha kwa viongozi na wadau wa madini kuhusu mswada wa kanuni za uanzishwaji masoko ya madini nchini inayofanyika jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu (kulia), wakiwa kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa Wilaya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu amepongeza nia njema ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha raslimali za taifa ikiwemo madini zinalinufaisha taifa, hivyo watendaji wanapaswa kuhakikisha wanamsaidia ili kutimiza nia hiyo.

Mtaturu aliyasema hayo jana jijini Mwanza baada ya kutamatika warsha ya siku mbili kwa viongozi na wadau wa madini kuhusu maudhui ya kanuni mpya za uanzishwaji masoko ya madini hapa nchini kama alivyoagiza Rais Magufuli hivi karibuni, iliyoandaliwa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na taasisi ya “Uongozi Institute”.

Warsha hiyo ilifunguliwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko ikiwashirikisha Maafisa Madini, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na viongozi wa wachimbaji wadogo wa madini kutoka mikoa ya Dodoma, Arusha, Geita, Shinyanga, Mara, Manyara, Njombe, Kagera, Tabora, Singida, Mbeya, Morogoro na Ruvuma.
Tazama BMG Online TV hapa chini 

No comments:

Powered by Blogger.