Header Ads

Mkutano Mkubwa wa Injili kufanyika Jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la "EAGT Lumala Mpya Internationa Church", Dkt. Daniel Moses Kulola anakukaribisha kwenye mkutano mkubwa wa injili wa OYES (Open Your Eyes and See) yaani Fungua Macho Yako na Uone kuanzia jumatatu 18.02.2019 hadi jumapili tarehe 24.02.2019.

Mchungaji Fred Mitchell pamoja na Mwinjilisti Wendy Smarty kutoka nchini Canada watahudumu kwenye mkutano huo kwa kushirikiana na wachungaji wenyeji pamoja na waimbaji na kwaya mbalimbali ikiwemo Havilah Gospel Singers, Revival Choir, New Salvation na Kaangae Choir.

Muda ni kuanzia saa tina mchana hadi saa kumi na mbili jioni katika viunga vya katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza. Walete wote wenye kuteseka na vifungo mbalimbali kwani kutakuwepo na huduma ya maombezi na kwa jina la Yesu watu wote watafunguliwa.

No comments:

Powered by Blogger.