LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mtazamo wa wachimbaji kuhusu Tanzania kuanzisha masoko ya madini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wizara ya Madini kwa kushirikiana na taasisi ya “UONGOZI Institute” imeandaa warsha kwa viongozi na wadau wa madini inayolenga kujadili maudhui ya kanuni mpya za uanzishwaji masoko ya madini hapa nchini kama alivyoagiza Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Warsha hiyo ya siku mbili ilifunguliwa jana jijini Mwanza na Waziri wa Madini, Doto Biteko ikiwashirikisha Maafisa Madini, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na viongozi wa wachimbaji wadogo wa madini kutoka mikoa ya Dodoma, Arusha, Geita, Shinyanga, Mara, Manyara, Njombe, Kagera, Tabora, Singida, Mbeya, Morogoro na Ruvuma.

BMG Online TV imezungumza na Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini mkoani Mara, David Bita ambaye anaeleza mtazamo wake kuhusiana na kanuni hizo za uanzishwaji masoko ya madini nchini ambazo zinaelezwa kwamba zitapunguza kero na malalamiko ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ikiwemo mlolongo wa kodi na tozo mbalimbali.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.