LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Wilaya Tunduru aeleza manufaa ya uanzishwaji masoko ya madini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera akizungumza na BMG kando ya warsha kwa viongozi na wadau wa madini kuhusu mswada wa kanuni za uanzishwaji masoko ya madini nchini inayofanyika jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wizara ya Madini kwa kushirikiana na taasisi ya “UONGOZI Institute” imeandaa warsha kwa viongozi na wadau wa madini inayolenga kujadili maudhui ya kanuni mpya za uanzishwaji masoko ya madini hapa nchini kama alivyoagiza Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
Warsha hiyo ya siku mbili ilifunguliwa jana jijini Mwanza na Waziri wa Madini, Doto Biteko ikiwashirikisha Maafisa Madini, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na viongozi wa wachimbaji wadogo wa madini kutoka mikoa ya Dodoma, Arusha, Geita, Shinyanga, Mara, Manyara, Njombe, Kagera, Tabora, Singida, Mbeya, Morogoro na Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera amezungumza na BMG Online TV na kubainisha mtazamo wake kuhusiana na kanuni hizo za uanzishwaji masoko ya madini nchini ambazo zinaelezwa kwamba zitapunguza utoroshwaji wa madini, kero na malalamiko ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ikiwemo mlolongo wa kodi na tozo mbalimbali.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.