LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wazazi na wanafunzi mkoani Geita waandamana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Maduka, Geita
Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Mchangani kilichopo katika Kijiji cha Ihumilo, Kata ya Nkome wilayani Geita, wameandamana wakishinikiza shule ya Msingi Rubondo ifunguliwe ili kuwaondolea adha watoto wao kutembea umbali mrefu wa kilomita tatu hadi Shule ya Msingi Nkombe kupata elimu.

Katika maandamano hayo ya amani, wazazi hao waliambatana na wanafunzi wakiwemo wanaosoma masomo ya awali, darasa la kwanza na darasa la pili ambao inaelezwa wanakumbana na changamoto ya kutembea umbali mrefu na kuhatarisha usalama wao ikiwemo ajali za mara kwa mara ambapo hadi sasa watoto watatu wamefariki dunia kwa kugongwa na pikipiki.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.