LIVE STREAM ADS

Header Ads

Sakata la utiririshaji maji yenye sumu lachukua sura mpya Nyamongo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiuliza mwisho wa mpaka wa eneo la ujenzi wa eneo la kuhifadhi maji yenye sufu (TSF) mpya katika mgodi wa Acacia North Mara uliopo wilayani Tarime. kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya Tarime.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu kulia) akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Mara pamoja na wawakilishi wa mgodi wa Acacia North Mara wakielekea kwenye eneo la uchimbaji wa shimo la kuhifadhia maji yenye sumu (TSF).
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mara, Adam Malima (wa kwanza kushoto) wakati akitoa taarifa fupi ya hali ya mkoa wake.


Na Issa Mtuwa, Wizara ya Madini 
Serikali imetishia kuufunga mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara ifikapo Machi 30, 2019 endapo mgodi huo utashindwa kuyadhibiti maji yenye sumu yanayo tiririka kutoka kwenye mabwawa ya kuhifadhia maji yenye sumu (Tailings Storage Facility -TSF) yanayotiririka kuelekea kwenye makazi ya wananchi.

Hayo yliesemwa Machi 5, 2019 na Waziri wa Madini, Doto Biteko alipotembelea mgodini hapo kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea mabwawa wa topesumu (TSF) na kuzungumza na uongozi wa mgodi na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nyamongo kuzungumzia hatima ya malipo ya fidia za wananchi waliohamishwa kupisha shuguli za mgodi huo.

Biteko alisema Serikali hairidhishwi na mgodi wa Acacia North Mara katika suala la uhifhadhi wa maji yenye sumu kwenye mabwawa yao. Alisema Serikali inathamini sana maisha ya watu na mtu mmoja mmoja na kwamba maisha ya mtu mmoja ni bora kuliko shuguli zote za mgodi.

"Naomba niseme ukweli, tena kutoka moyoni, sijaridhishwa na hili jambo la utiririshaji wa maji yenye sumu kuelekea kwenye makazi ya watu. Serikali hii ya awamu ya tano ya Dkt. John Pombe Magufuli inathamini sana maisha ya watu wake kuliko kitu chochote. Thamani ya maisha ya mtanzania mmoja ni bora kuliko kinachochimbwa hapa. Nitoe rai kwa mgodi ifikapo Machi 30, mwaka huu, hili jambo liwe limekwisha, kinyume cha hapo, nitafunga mgodi mpaka pale mtakapo tekeleza jambo hili". Alisema Biteko.

Katika ziara hiyo, Waziri Biteko aliambatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo akiwemo Kamishna wa Madini Mhandishi David Mlabwa na Afisa Madini Mkoa Mara Mhandisi Nyaisara Mgaya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Mara ikiongwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa Mara, Adam Kigoma Malima.

Ziara hiyo inafuatia vikao mbalimbali vya awali vilivyofanyika mwaka huu vikilenga masuala mbalimbali yanayohusu mgodi huo ikiwemo suala la udhibiti wa maji yenye sumu (topesumu) yanayolalamikiwa na wananchi wanaoishi jirani mgodi huo, kikao cha kwanza kilifanyika Januari 19, 2019 chini ya Makatibu Wakuu wa Wizara saba ((Wizara ya Madini, Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano-Baraza la Taifa la Mazingira NEMC, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Maji pamoja na Wizara ya Fedha).

No comments:

Powered by Blogger.