LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko akerwa na tabia ya uongozi wa Acacia North Mara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiongea na wananchi kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamongo wilayani Tarime, Machi 05, 2019.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (wa kwanza kulia) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Nyamongo wilayani Tarime, katikati yao ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Charles Kabeho.

Na Issa Mtuwa – Wizara ya Madini, Tarime
Waziri wa madini, Doto Biteko ameonyesha kukerwa na tabia ya uongozi wa juu wa mgodi wa Acacia North Mara kwa serikali kwa kushindwa kuhudhuria vikao mbalimbali vinavyo andaliwa baina ya pande hizo mbili, licha ya baadhi ya vikao kuongozwa na Waziri wa Madini lakini viongozi wa juu wa mgodi huo ambao ndio wafanya maamuzi na watekelezaji wa maagizo ya serikali wamekuwa wakishindwa kuhudhuria .

Biteko alisema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara Machi 5, 2019 katika eneo la Nyamongo wilayani Tarimena kuongeza kwamba anakerwa na tabia za uongozi wa mgodi huo kwa kushindwa kuhudhuria mara kwa mara mikutano mbalimbali ya ndani na ile ya hadhara badala yake wamekuwa wakituma wawakilishi.

“Kuanzia leo, haki ya Mungu, haki ya Mungu, haki ya Mungu, mimi Waziri wa Madini leo ni siku ya mwisho kukaa na hawa wawakilishi kwenye vikao, hasa kama hivi vinavyo husu hatima ya maisha ya watu halafu wafanya maamuzi hawahudhurii. Niwambie ukweli nasikitishwa sana na tabia hii. Hawa waliopo sio saizi yangu, kama ni hawa hata mimi ningewaleta Maafisa wa Wizara tena wale wanaolingana na hawa.

"Wanataka wawepo hadi afike Rais…!? nendeni mkawambie kwenye ngazi ya Wizara mimi ndio wa mwisho katika kufanya maamuzi, kama mimi nipo kwa nini wao wasiwepoo…!? nyinyi mliokuja hapa nendeni mkawaambie hii ni mara ya mwisho wasifikiri Serikali hii wanaweza kuiweka mfukoni, haikubaliki, hii tabia lazima ifike mwisho". Alisema Biteko.

Alisema kwa ujumla hafurahishwi na namna mambo yanavyokwenda mgodini hapo ukilinganisha na migodi mingine. Mgodi wa North Mara umezungukwa na matatizo mengi yakiwemo ya malipo yafidia za wananchi, utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya wananchi.

No comments:

Powered by Blogger.