LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mikakati yazidi kupamba moto ili kutokomeza ziro wilayani Kisarawe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya Tokomeza Ziro wilayani humo.
Na Fredy Njenje
Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kutoka kushoto) akipata maelekezo katika moja ya maabara wilayani Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwigelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kulia) akigawa vifaa vya shule ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Tokomeza Ziro wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Makurunge.
Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi.


Tokomeza Ziro Kisarawe ni kampeni maalum kwa ajili ya kuongeza ufaulu na kuondoa kabisa ziro katika Wilaya Kisarawe mkoani Pwani. Changamoto wanazopitia walimu na wanafunzi ni nyingi. Elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo wana Kisarawe wameona ni vyema kuwekeza katika Elimu.

"Ukimsaidia mtoto akapata elimu unakuwa umeweza kusaidia Tanzania nzima na mimi kuanzia sasa nataka tuanze na kidato cha nne na sita tufute hizo zero na zisiwepo kabisa. Katika kuhakikisha hili linatimia kuna mambo mengi ambayo tutafanya kwa kushirikiana na wadau wote wa elimu nchini". Alisema Mwegelo.

Mwaka jana kampeni hii ya Tokomeza Ziro ilifanyika kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwa kuongeza ufaulu ikiwa ni kupunguza ziro kutokea 455 mpaka 259 na kuondoa ziro kabisa kwa kidato cha sita.

Kwa kuona hili, Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwegelo alizindua kampeni dada ijulikanayo kama "Tokomeza Zero" Kisarawe ikijumuisha wanafunzi kuwekwa kwenye kambi kwa ajili ya mafunzo maalum, uboreshwaji wa miundo mbinu mashuleni, elimu na kozi kwa waalimu ili kuinua kiwango cha elimu wilayani Kisarawe.

Utafiti unaonyesha wanafunzi wengi wa Kisarawe hutembea umbali mrefu kwenda shule (zaidi ya kilomita 15 kwenda pekee) hali inayofanya wanafunzi kufika shuleni wakiwa wamechoka, mtoto wa kike ambaye atahitajika kufanya usafi nyumbani kisha aende shule kwa kutembea huchoka zaidi.

Miundo mbinu ya shule ni changamoto na hata idadi za shule wilayani Kisarawe ni chache kwa kulitambua hilo, kuna ushirikishwaji wa wadau wa elimu ili kuwezesha ujenzi wa shule kwa ajili ya wana Kisarawe na mkazo unawekwa zaidi ili kufanikisha kampeni ya "Tokomeza Zero".

"Wanafunzi wote wa Kisarawe wa kidato cha nne na cha Sita watapata mafunzo ya ziada ili kujiandaa na mitihani yao ya taifa ili kuwaepusha na kazi za kila mara wanafunzi hawa watakuwa kwenye kambi maalum kwa muda miezi miwili kabla ya muda wa mitihani yao ya Taifa." Alisema Mwegelo.

Sambamba na hilo waalimu wanapatiwa mahitaji yote muhimu ili kufanikisha zoezi lao la ufundishaji na pia kuboresha miundo mbinu ya shule ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi na walimu.

Ili kufanikisha kampeni hii, imeandaliwa "Dinner Gala" tarehe 30/03/2019 Ukumbi wa Mlimani City, katika jitihada za kukusanya fedha ambazo zitatumika katika ujenzi ya mabweni, shule hiyo itakuwa na madarasa ya kutosha, maktaba pamoja na maabara za kisasa. Shule hiyo itakuwa ya kwanza ya aina yake Kisarawe na kama mdau wa elimu unaweza kushiriki kwa kuchangia Tsh 100,000 au kununua meza moja kwa shiling million moja . 

Fedha zote hizo zitaelekezwa katika ujenzi wa shule hiyo ya kwanza ya aina yake yenye lengo la kuwa shule ya mfano ambapo shule zitakazofuatia zitaundwa kwa mfano huo. Unaweza kushiriki kwa kupiga simu nambari 0677 062 070 au 0656 132 676 kupata tiketi.

No comments:

Powered by Blogger.