LIVE STREAM ADS

Header Ads

Askofu makanisa ya "Last Church Tanzania" ataka viongozi wa dini kuisaka elimu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Joel Maduka, Geita
Askofu Mkuu wa Makanisa ya "Last Church" nchini Tanzania, Japhet Wanzagi amewataka watumishi wa Mungu kuwekeza nguvu kubwa zaidi kuitafuta elimu kwani ndiyo ufunguo pekee ambao utawasaidia kuwaongoza vyema waumini wao na kuendana na mfumo wa sasa wa Sayansi na teknolojia.

Aliyasema hayo kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Biblia cha Victoria kilichopo mkoani Geita ambapo wahitimu walitunukiwa vyeti ngazi ya Stashahada ya Diplomasia ya Theolojia chuoni hapo.

"Tunatambua katika ulimwengu wa sasa hakuna jambo lililo jema kama kwa viongozi wa dini, wachungaji na mashemasi kujiendeleza kielimu na kuachana na dhana ya kwamba elimu ni ya watu wengine na kuona kwamba kwa kuwa wao wanafanya kazi za utume na sio lazima kusoma". Alisema Askofu Wanzagi.
Naye Mwl. Martha Mkondo aliwahimiza wahitimu wa chuo hicho kutambua kuwa elimu haina mwisho na kwamba jambo ambalo wamelichagua ni zuri na la kupongezwa na kila mtu.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Mch. Joseph Hewa alisema kimejikita kufundisha zaidi neno la Mungu pekee na kwamba hawana desturi ya kuchanganya mafundisho na masomo mengine kama ilivyo kwa baadhi ya vyuo vya biblia.

Jumla ya wanafunzi tisa walihitimu masomo ya Theolojia kwa ngazi ya Stashahada na kutunukiwa vyeti.

No comments:

Powered by Blogger.