LIVE STREAM ADS

Header Ads

Idadi ya vifo yaongezeka ajali ya "Coaster" Mwanza, majeruhi waanza kuruhusiwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Alhamisi Aprili 18, 2019 majira ya saa saba mchana, watu wawili walifariki dunia huku wengine 18 wakijeruhiwa baada ya basi dogo la abiria (Coaster), lililokuwa linafanya safari zake kati ya Mwanza mjini na Igombe wilayani Ilemela kupasuka tairi na kutumbukia mtaroni katika barabara ya Igombe jirani na uwanja wa ndege wa Mwanza.

Majeruhi katika ajali hiyo inayoelezwa kuwa chanzo chake ni mwendo kasi wakati ambapo dereva alikuwa akijaribu kulipita lori walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo inaelezwa kwamba idadi ya vifo iliongezeka baada ya usiku wa kuamkia jana Aprili 19, 2019 majeruhi mmoja kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Bugando na hivyo kufanya idadi kufikia vifo kufikia watu watatu. Aidha Majeruhi wengine hali zao zinaendelea vyema na tayari wameanza kuruhusiwa kutoka hospitalini.
#BMGHabari
Baadhi ya wakazi wa Igombe wameomba vyombo vya usalama hususani jeshi la polisi kuongeza idadi ya askari usalama barabarani katika barabara hiyo kwani baadhi ya madereva wamekuwa wakiendesha kwa mwendo wa kasi.
Baadhi ya mashuhuda wanashauri pia ukaguzi wa magari ya Mwanza-Igomba kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara kwani baadhi yake yamekuwa na hitilafu.
Inaelezwa Coaster hiyo ilipasuka tairi ya mbele hali iliyosababisha kutumbukia mwenye mtaro.
BMG tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na ajali hii. Tunawaombea majeruhi wote wapate ahueni mapema na waliopoteza maisha Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, Amina!

No comments:

Powered by Blogger.