Header Ads

Uongozi Lipuli FC waitisha harambee kuinurusu timu na madeni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kaimu Mwenyekiti wa timu ya soka ya Lipuli FC ya mkoani Iringa, Ayoub Kihwelo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee ya kuchangia timu hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Iringa wakiwasikiliza viongozi wa timu ya Lipuli FC.

Na Fredy Mgunda, Iringa
Uongozi wa timu ya mpira wa miguu Lipuli FC ya mkoani Iringa inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara mepanga kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo kwa lengo la kuimarisha uchumi ili kutatua changamoto za mishahara pamoja ada za wachezaji ambazo hadi sasa wanadaiwa.

Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo, Ayoub Kihwelo amesema kuwa lengo la kuitisha harambee hiyo ni kufanikisha kupata fedha za kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo klabu inadaiwa na wachezaji na pia kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.

Kihwelo aliongeza kuwa harambee hiyo itafanyika Jumapili Aprili 07, 2019 katika ukumbi wa kichangani uliopo Manispaa ya Iringa ambapo wanatarajia Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Mizengo Pinda kuwa mgeni rasmi.

Kihwelo alisema wanatarajia kupata zaidi ya shilingi milioni mia tatu kwenye harambee hiyo, fedha ambazo zitasaidia kuendesha timu bila kuwa na deni lolote kutoka kwa wachezaji huku pia ikifanya usajili mpya wa msimu ujao.

"Tunalipa zaidi ya shilingi milioni 24 kila mwezi kwa ajili ya mishahara tu ya wachezaji wa timu na tunagharamia zaidi ya shilingi 300,000 kwa siku kwa ajili ya kambi ya timu hivyo utaona kwa namna gani timu inavyogharimu kiasi kikubwa cha fedha na hadi hivi sasa timu haina mdhamini yeyete yule". Alisema Kihwelo

Naye Katibu Mkuu Lipuli FC, Julius Leo ameomba wananchi, wadau wa soka na wapenzi wa klabu hiyo kuichangia kwa kutumia akaunti ya benki ya CRDB 01J2072252000 ama kupitia namba ya M-Pesa 0744 16 24 46 jina Lipuli FC.

No comments:

Powered by Blogger.