LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko afanya mazungumzo na viongozi mbalimbali Jijini Dodoma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali alipokutana na Mkurugenzi wa Biashara na Uendeshaji wa Masoko kutoka kampuni ya MAGUL Security System, Michael Gur Arie Jijini odoma.
Waziri Doto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka kampuni ya MAGUL Security System.
Waziri Doto Biteko akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Wachimbaji nchini (FEMATA), John Bina (kulia) wakati wa mazungumzo yao ofisini kwake Dodoma. Kushoto ni Mtendaji mkuu wa Shrikisho hilo ambaye pia ni Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega.
Waziri Doto Biteko akiongea na viongozi wakuu wa Shirikisho la Wachimbaji nchini (FEMATA).
Waziri Doto Biteko katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Wachimbaji nchini (FEMATA).

Na Issa Mtuwa, Dodoma
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na makundi mbalimbali ya wadau wa madini ofisini kwake Jijini Dodoma.

Miongoni mwa aliokutana nao ni pamoja na kampuni ya MAGAL Security System inayojihusisha na ufungaji wa mitambo ya usalama (security system) katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya migodini.

Mkurugenzi wa Biashara na Uendelezaji wa Masoko wa kampuni hiyo, Michael Gur Arie, alimweleza Waziri kuwa, kampuni yake inataka kufanya kazi na Wizara ya madini katika masuala ya ufungaji wa mitambo ya usalama kwenye migodi hususani Mirerani.

Alisema kuwa, kampuni hiyo ina uwezo wa kufunga mitambo Mirerani na wizara ikawa na uwezo wa kufuatilia kinacho fanyika kwenye eneo lote la mgodi huku shughuli nyingine za ofisi zikiendelea.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko aliiishukru kampuni ya MAGAL kwa kumtembelea na kuzungumza nae kuhusu suala la usalama hususani Mirerani. Amesema suala la usalama mirerani linapewa kipaumbele na uzito mkubwa katika kulinda raslimali hiyo ili iwanufaishe Watanzania wote.

Aliongeza kuwa serikali imelipa kipaumbele suala la usalama katika eneo la Mirerani na Wizara imekuwa na mpango wa awamu mbili katika kutekeleza suala hilo. Amesema, Awamu ya kwanza ilikuwa ni kujenga ukuta kuzunguka eneo lote la migodi ya Mirerani na kufunga kamera na awamu ya pili inasubiri ushauri wa namna ya kutekeleza huku utekelezaaji wake ukitarajiwa kutafanyika baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Waziri Biteko amekutana na viongozi wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Nchini (FEMATA) wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo, John Bina.

Bina na ujumbe wake walimtembelea Waziri Biteko kwa lengo la kukutana na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu shirikisho hilo ukizingatia kwamba, tangu ateuliwe kushika wadhifa huo hawajawahi kukutana na kufanya mazungumzo rasmi zaidi ya kukutana kwenye ziara mbalimbali.

Bina alimweleza Waziri kuwa Shirikisho lina laani vikali tukio la udanganyifu uliotokea hivi majuzi huko Chunya na kuongeza kwamba FEMATA haikubaliana na udanganyifu unaofanywa na wachimbaji kwa kushirikiana na baadhi watendaji wa serikali waliopewa dhamana na kwamba halipo tayari kuwalinda wala kuwateteta.

Pia Bina alizungumzia kuhusu mgodi wa Buhemba uliofungwa na Serikali akimuomba Waziri kuufugua mgodi huo kwani wanachi wengi walio katika eneo hilo wanategemea maisha yao kutokana na uwepo wa mgodi huo.

Aidha alimwomba Waziri maeneo mbalimbali yanayochukuliwa na Serikali afikirie kuwapatia wawekezaji wazawa ili wayaendeleze kwa shughuli za uchimbaji. Bina aliongeza kuwa FEMATA ina mpango wa kuanzisha Benki ya Wachimbaji (Miners Bank) kwa ajili ya kuwahudumia wachimbaji nchini.

Kwa upande wake, Waziri Biteko alimshukru Rais wa FEMATA na ujumbe wake kwa kumtembelea. Alisema FEMATA na Wizara ya Madini huwezi kutenganisha kwa kupiga mstari kwa kuwa watu wa FEMATA ndio wadau wa wizara na kwamba hawajawahi kutofautiana na kuomba ushirikiano huo uendelee.

Vilevile Biteko aliwashukru FEMATA kwa kuunga mkono na kulaani kitendo cha udanganyifu uliofanywa na wachimbaji kwa kushirikiana na watendaji wa wizara huko Chunya kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu uzalishaji wa madini.

Kuhusu kufunguliwa kwa mgodi wa Buhemba, Biteko alisema Wizara inathamini maisha ya watu kuliko shuguli za uchimbaji na kuongeza kwamba hivi sasa kuna timu ya wataalamu ambao wamekwenda Buhemba kufuatilia utekelezaji wa waliyokubaliana katika kikao cha Machi 06, 2019, na ripoti hiyo inategemewa kuwa mwongozo wa iwapo mgodi huo ufunguliwe au ufungwe.

Akizungumzia kuhusu uanzishwaji wa Benki ya Wachimbaji amesema ni jambo zuri na kushauri kuanza na SACCOS ili kupima imani ya uaminifu wa wanchama wake katika kurejesha amana watakazo kuwa wanakopa.

Waziri Biteko aliwahakikishia FEMATA kuwa wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yake.

No comments:

Powered by Blogger.