Taasisi ya MOI yaendesha kambi kubwa ya upasauji Jijini Mwanza
zYaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Dkt. Philis
Nyimbi akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya
kufunga kambi ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando Jijini Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI, Dkt. Respicious Boniface akieleza namna taasisi hiyo ilivyojipanga kusogeza huduma kwa
wananchi kwa kufanya kambi za uapasuaji, katika hafla ya kufunga kambi ya
Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu iliyofanyika Bugando.
1Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya
Bugando, Profesa Abel Makubi akitoa taarifa ya namna kambi ya
upasuaji iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya MOI, Bugando na Cuba
ilivyafanikiwa
Mdaktari Bingwa wa MOI, Cuba pamoja na
Bugando wakifanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo.
Zaidi ya wagonjwa 400 wamehudumiwa kati yao 17 wakifanyiwa upasuaji mkubwa na jopo la madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI,Cuba na Bugando katika kambi ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu katika Hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza kuanzia tarehe 8/04/2019 hadi 12/04/2019.
Akihitimisha kambi hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dkt.Philis Nyimbi amemshukru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya maboresho makubwa hapa nchini hususani kwenye huduma za Afya.
"Kambi hii ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu imewezakana kutokana na Maboresho yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya Tano, kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu John Mongela tunawashukuru wakurugenzi wakuu wa MOI na Bugando pamoja na madaktari Bingwa wote, kwa hili wananchi wa kanda ya ziwa wamenufaika sana". Alisema Dkt Nyimbi
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface alisema hii ni sehemu ya mkakati wa MOI na Serikali wa kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia wananchi wote hususani wa mikoa ya pembezoni.
"Baada ya Serikali kufanya uwekezaji mkubwa MOI ,rufaa za nje ya nchi zimepungua sana, hivi sasa mpango wa MOI na Serikali ni kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia wananchi wote". Alisema Dkt. Boniface.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Bugando, Profesa Abel Makubi aliushukuru Uongozi wa MOI kwa kukubali kuleta madaktari Bingwa Mwanza ambao wamewahudumia wakazi wa kanda ya ziwa na kuwapunguzia adha ya kusafiri kwenda Dar es Salaam au nje ya nchi.
"kwa niaba ya bodi pamoja na menejimenti ya Hospitali ya Bugando tunawashukuru wenzetu wa MOI,Cuba kwa kuja kushirikiana nasi hapa kwenye kambi hii, tunaamini huu ni mwanzo wa ushirikiano baina ya taasisi zetu wakazi wa kanda ya ziwa wataendelea kunufaika". Alisema Profesa Makubi.
Taasisi ya MOI imekuwa ikitekeleza kwa vitendo maagizo ya Serikali ya kuhakikisha inawaogezea wananchi wa mikoa ya pembezoni huduma za kibingwa ili kuwapunguzia adha kusafiri kuzifuata huduma hizo MOI.
No comments: