LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Shinyanga yachangia damu na kufanya usafi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa Shinyanga (Ahmadiyya Muslim Jamaat) wakiongozwa na vijana wa jumuiya hiyo wamejitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wahitaji hususani akina mama na watoto katika Zahanati ya Nhelegani iliyopo katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga. 
Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha Afya Kambarage, Devotha Omary (kushoto) akiandika jina la Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko (wa pili kushoto mwenye kanzu ya bluu) baada ya kumpima wingi wa damu wakati wa zoezi la utoaji damu katika Zahanati ya Nhelegani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Sheikh Yusuph Mgeleka (kulia) akipimwa presha wakati wa zoezi la uchangiaji damu.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko akitoa damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya mama, mtoto pamoja na watu wengine wenye uhitaji wa damu.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha Afya Kambarage, Lucy Biseko akimhudumia Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko baada ya kumaliza kutoa damu.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha Afya Kambarage, Lucy Biseko akimwandaa Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Abdulghani Msimba ili atoe damu.
Mganga katika Zahanati ya Nhelegani, Johanes Barnabas akiendelea na zoezi la kuwapima presha vijana wa Ahmadiyya waliojitolea kuchangia damu.
Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Sheikh Yusuph Mgeleka akigawa vinywaji katika Zahanati ya Nhelegani.
Vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakifyeka nyasi katika zahanati ya Nhelegani.
Vijana wakiendelea na usafi.
Picha ya kumbukumbu : Viongozi na vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kufanya usafi katika Zahanati ya Nhelegani.
Picha ya pamoja baada ya kumaliza kufanya usafi katika Zahanati ya Nhelegani.
Viongozi na vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakisali na kufanya ibada ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Sheikh Yusuph Mgeleka baada ya kumaliza kchangia damu na kufanya usafi katika Zahanati ya Nhelegani.

Na Kadama Malunde - Malunde1 Blog
Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa Shinyanga (Ahmadiyya Muslim Jamaat) wakiongozwa na vijana wa jumuiya hiyo wamejitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wahitaji hususani akina mama na watoto katika Zahanati ya Nhelegani iliyopo katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.

Zoezi hilo la uchangiaji damu lilifanyika jana ambapo mbali na kuchangia damu vijana hao wamesafisha mazingira katika zahanati hiyo kwa kufyeka nyasi na kuzoa taka.

Rais/ Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka alisema wameamua kuchangia damu ili kunusuru maisha ya mama na mtoto lakini pia kufanya usafi ili kuweka mazingira ya zanahati ya Nhelegani kuwa salama.

“Tumehamasishana kufanya shughuli hizi kwa mikono yetu,hali hii ya kujitolea inajulikana kwa jina la‘Waqar Amal’ ikiwa na maana ya kujitolea kusaidia kwa mikono yako mwenyewe,utoke jasho mwenyewe, hili ni zoezi endelevu tumekuwa tukijitolea katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga na maeneo mengine duniani”,alieleza Sheikh Mgeleka.

“Tunafanya popote na hatubagui kwa ajili ya manufaa ya viumbe vya Mwenyezi Mungu na hii ni sehemu ya mafundisho ya dini Tukufu ya Islam,malipo ya jasho letu ni mbele ya Mungu na haya ndiyo mafundisho muhimu ambayo daima tunatakiwa kukumbushana kwa ajili ya kusaidia viumbe wenzetu,pia tumefundishwa kuwa kujitolea ni heshima”,alisema Sheikh Mgeleka.

Naye Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko alisema zoezi la kuchangia damu ni huduma kwa viumbe ijulikanayo kwa jina la ‘Khidmatil Khalqi’ ikiwa ni utekelezaji wa kauli mbiu ya Ahmadiyya ya ‘Upendo kwa wote bila chuki kwa yeyote’.

“Zoezi hili limeshirikisha vijana wa Ahmadiyya mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Masheikh wa matawi mbalimbali wakionesha mfano kwa waumini tunaowaongoza, hili ni agizo la Kiongozi wetu Mtukufu Duniani Hazrat Mirza Masroor A.T.B.A Khalifatul Masihi wa tano kusaidia viumbe wenzetu”,alisema Sheikh Gesonko.

“Tunatoa huduma kwa yeyote aliyepata shida ili apate uhai,tumeleta huduma hii kwenye zahanati inayosimamiwa na serikali kwa sababu serikali ndiyo wanahusika na majanga na huduma mbalimbali za binadamu hasa afya,na tumekuwa tukichangia damu hata kwenye mikutano yetu mikuu mwezi Septemba kila mwaka”,alisema Sheikh Gesonko.

No comments:

Powered by Blogger.