Header Ads

Wadau waombwa kuinusuru timu ya "Cricket" inayoshiriki kombe la dunia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Timu ya watoto kutoka taasisi ya "Pamoja Child and Youth Foundaton" ya Jijini Mwanza imepata fursa ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kwanza ya kombe la duni la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu/ wanaotoka mitaani kwenye mchezo wa Cricket nchini Uingereza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Changamoto kubwa ni ukata kuikabili taasisi hiyo kwa ajili ya maandalizi ya kuisafirisha timu pamoja na kuhakikisha ushindi upatikana hivyo wadau mbalimbali wamehimizwa kutoa ushirikiano wao wa hali na mali.
Itakumbukwa timu za watoto wanaotoka mitaani zimekuwa zikifanya vizuri kwenye mashindano ya kombe la dunia la watoto wanaotoka mtaani hivyo awamu hii pia ni fursa kwa Tanzania kwani ndiyo nchi pekee imetoa timu katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Hapa timu hiyo ya watoto ya Cricket ilikuwa ikijinoa kwenye bonanza la michezo lililofanyika Machi 30, 2019 katika shule ya sekondari Isamilo International huku kiingilio kikipelekwa kwa timu kwa ajili ya maandalizi.
Tazama BMG Online TV hapa chini kwa undani zaidi

Charity Event at Pamoja Child and Youth Foundation

Wanafunzi wa CUHAS Mwanza wamuunga mkono kijana Raphael Swai
#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.