LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau wakutana Morogoro kutafuta suluhu ya changamoto za sekta ya habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwanza Afrika MISA tawi la Tanzania (MISA Tanzania) kwa kushirikiana na Shirika la  International Media Support (IMS) linalojikita katika kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari ili kupunguza migogoro, kuimarisha demokrasia na kuwezesha uhuru wa kupata taarifa imewakutanisha wadau mbalimbali katika semina ya kujadili mazingira yaliyopo ya vyombo vya habari na kupendekeza namna ya kuzikabili changamoto zinazodumaza sekta ya habari na uhuru wa kujieleza nchini.

Warsha hiyo ya siku mbili iliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro iliwakutanisha wawakilishi na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari ikiwemo waandishi wa habari, asasi za kiraia, wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu.

Washiriki hao walisema kutokuwa na umoja thabiti na nia ya pamoja ndio imekuwa chanzo kikuu cha matatizo mengine kunawiri na kupendekeza kuwa kabla ya kutafuta suluhu nyingine, mkazo uwekwe katika kuwa na umoja thabiti na nia ya pamoja miongoni mwa wadau wote wa tasnia ya habari.
Mwakilishi kutoka Shirika la  International Media Support (IMS) akielezea umuhimu wa ushirikishwaji kwa kila mdau katika mchakato wa kukuza sekta ya habari na uhuru wa kujieleza.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Alex Benson (wa kwanza kushoto aliyeketi) akielezea umuhimu wa wanahabari kuwa na uelewa wa kanuni zinazowasimamia ili kuepuka kuzikiuka mara kwa mara.
Wakili James Marenga akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo.
Dr. Geofrey Chambua ambaye ni mshauri wa maendeleo na sheria akielezea uzoefu wake katika kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali kutatua changamoto za kimaendeleo.
Mwandishi wa habari wa kujitegemea kutoka Zanzibar, Ali Othman akichangia mawazo katika warsha hiyo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St. John (SMC), Michael Gwimile akichangia mada katika warsha hiyo.
Joyce Shebe ambaye ni mhariri Clouds Media akiwasilisha mada kwa niaba ya kundi la majadiliano katika warsha hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva akizungumza kwenye warsha hiyo.

Taasisi ya MISA Tanzania yatoa mafunzo kwa wanahabari mkoani Simiyu
#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.