Header Ads

Shirika la HAKI ZETU lasisitiza huduma bora za afya kupambana na vifo vya uzazi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, BMG
Ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa wanawake, inapaswa majengo ya vituo vya kutolea huduma za afya yaendane sambamba na utoaji bora wa huduma, vifaa tiba, watoa huduma na mazingira rafiki.

Hayo yalisemwa na Meneja Mradi kiutoka shirika la Haki Zetu, Evodius Gervas wakati akizungumzia mradi wa Ishi Vizuri Sasa awamu ya pili (Living Better Today Phase II) unaojumuisha programu ya afya ya uzazi ili kuelimisha jamii kuhusu huduma na taarifa sahihi za afya hususani kwa wamama wajawazito.

Gervas alisema licha ya Serikali kufanya jitihada za kujenga na kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya, kumekuwepo na wanawake wengi ambao wajifungulia nyumbani pamoja na kutofuata huduma za afya hali inayopelekea ongezeko la vifo vya kinamama vinavyotokana na uzazi kwani wanakosa taarifa sahihi kuhusu afya zao na maendeleo ya mtoto kabla ya kuzaliwa.

Alisema shirika la Haki Zetu lilianzisha programu hiyo ambayo lengo lake ni kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa huduma za afya kwa wajawazito pamoja na kuwapa taarifa sahihi kuhusu huduma za afya ikiwemo kumuona mtaalamu wa afya kwa uchunguzi zaidi, kuhudhuria kliniki na kujifungulia hospitalini.

Vituo binafsi vya Afya Mwanza kutoa huduma bure kwa wananchi
#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.