LIVE STREAM ADS

Header Ads

Magari yanayouza maji yaanza kusajiliwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Afisa Mawasiliano wa DAWASA ,Joseph Mkonyi (kulia) akitoa maelekezo kwa dereva baada ya kumaliza zoezi la ubandikaji wa stika ili kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano wa DAWASA, Joseph Mkonyi (kulia) akitoa cheti cha utambuzi kwa dereva baada ya kumaliza zoezi la ubandikaji wa stika ili kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/ MMG
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kutekeleza zoezi la usajili na utoaji wa vibali kwa magari ya kusambaza majisafi (water Bowsers) katika jiji hilo pamoja na Pwani.

Zoezi hilo litaendeshwa kwa wiki mbili kuanzia Mei 15, 2019 hadi Mei 29, 2019 katika eneo la Kituo cha Chuo Kikuu cha Ardhi chenye matanki ya DAWASA maarufu kama Terminal, Tegeta na Bagamoyo.

Afisa Mawasiliano wa DAWASA, Joseph Mkonyi alisema kuwa zoezi hilo linalengo la kuwatambua wauzaji wote wa majisafi ikiwa na kuangalia usalama wa vyombo wanavyotumia kuwauzia maji wananchi.

"Niwaombe wote wenye kufanyabiashara ya majisafi kujitokeza ili tuweze kuwatambua na kuwapa leseni na kuwapa mikakati yenye lengo la kujenga ili watoe huduma salama," alisema Mkonyi.

Zoezi hilo la usajili linamtaka mwenye gari kuja na vielelezo ikiwemo picha moja ya rangi ya mmiliki wa gari na nakala ya kitambulisho chake (KURA, UTAIFA au HATI YA KUSAFIRIA).

Kingine ni nakala ya kasi ya gari, nakala ya bima ya gari na nakala ya leseni ya dereva vyote viwe vimethibitishwa na mwanasheria.

Alisema kuwa matenki yatakayokuwa yamekidhi vigezo vya kupata usajili yatasafishwa na dawa maalumu ya kuua wadudu kwenye mantenki na kubandikwa stika ya DAWASA.

Alisisitiza kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika Mei 29, 2019 gari litakalokuwa halijasajiliwa halitaruhusiwa kuendesha biashara ya kutoa huduma ya kuuza maji na wananchi wanashauriwa kutoa taarifa endapo wataona magari hayo yakitoa huduma bila kuwa na vibali ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

No comments:

Powered by Blogger.