LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenge wa Uhuru waridhia miradi sita wilayani Sengerema, miwili yakataliwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mwenge wa Uhuru 2019 umepitia miradi minane ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya Sengerema mkoani Mwanza na kuridhishwa na miradi sita huku miradi miwili ikiingia dosari kutokana na mkanganyiko wa taarifa za utekelezaji wake.

Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo zilifanyika jana Mei 15, 2019 ambapo miradi iliyokubaliwa ni mradi wa maji Kijiji cha Busisi, kisima kirefu Nyamasale, klabu ya kupinga rushwa katika Shule ya Sekondari Lusikwe, ujenzi wa Shule ya Msingi Kachuo, maabara ya uzalishaji vifaranga vya samaki Chamabanda huku miradi iliyokataliwa ikiwa ni ujenzi wa jengo la wazazi katika Zahanati ya Kasenyi pamoja na barabara ya Igaka-Buzilasoga kwa kiwango cha moramu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema, Mhandisi Nickas Ligombe (pichani) alisema mradi wa maji katika Kijiji cha Busisi umegharimu shilingi Milioni 486 ukitarajiwa kuwanufaisha wakazi zaidi ya 6,000 utakapokamilima mwishoni mwa mwezi huu.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitafa, Mzee Mkongea Ali pamoja na timu yake akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Kijiji cha Busisi.
Mwenge wa Uhuru 2019 ulikagua uendelevu wa mradi wa maji wa kisima kirefu Nyamasale na kuridhishwa na mradi huo ambao umesaidia kuondoa adha ya upatikanaji maji kwa wananchi.
Mwenge wa Uhuru 2019 wilayani Sengerema.
Mwenge wa Uhuru 2019 uliridhia ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Kachuo katika Kata ya Matongo na kuweka jiwe la msingi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali akizungumza alipowasili katika Kata ya Matongo akiwa na timu yake.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Shule ya Msingi Kachuo.
Shule ya Msingi Kachuo inajengwa kwa nguvu za wananchi, Halmashauri ya Sengerema pamoja na wahisani mbalimbali.
Msimamizi wa mradi wa maabara ya kuzalisha vifaranga vya samaki Chamabanda akitoa taarifa ya mradi huo ambapo alisema utasaidia kupambana na uvuvi haramu pamoja na uhifhadhi wa mazingira.
Mwanahabari (kushot) akiwa kwenye mahojiano na wakazi wa Sengerema.
Mradi wa kuzalisha vifaranga vya samaki aina ya Sato.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali na timu yake akiwa kwenye mradi wa kuzalisha vifaranga vya samaki Chamabanda wilayani Sengerema.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali aligoma kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la wazazi katika Zahanati ya Kasenyi ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi milioni 63, hadi sasa limegharimu shilingi milioni 36.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali pamoja na timu yake akikagua urefu wa barabara ya Igaka-Buzilasoga wilayani Sengerema iliyokarabatiwa kwa kiwango cha moramu kutokana na ukosefu wa nyaraka kadhaa zinazodhihirisha ubora wake.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.