LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakazi wa Kasisa Halmashauri ya Buchosa wapata shule

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Jana Mei 16, 2019 mbio za Mwenge wa Uhuru zimepitia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu, miundombinu ya barabara pamoja na maji. Kwa upande wa mradi wa elimu, Mwenge wa Uhuru ulizindua Shule mpya ya Sekondari Kata ya Kasisa na hivyo kuondoa adha ya wanafunzi katika Kata hiyo kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.
#BMGHabari
Mkuu wa Idara ya Mipango Halmashauri ya Wilaya Sengerema, Ndaro Samson (kushoto), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kaimu Mkuu wa Wilaya Sengerema, Joseph Kapunda (kulia) kwa ajili ya kukimbizwa katika Halmashauri ya Buchosa.
Viongozi mbalimbali wakiulaki Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.
Viongozi mbalimbali wakiwa tayari kuulaki Mwenge wa Uhuru 2019 katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.