LIVE STREAM ADS

Header Ads

PICHA- Mwenge wa Uhuru ukiwasili wilayani Sengerema

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 ukiwasili katika eneo la Kigongo Feri wilayani Misungwi ili kuvuka maji kuelekea eneo la Busisi wilayani Sengerema kwa ajili ya kuanza mbio zake kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo, jumatano Mei 15, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Ukiwa wilayani Sengerema, Mwenge wa Uhuru unapitia miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.78 ambapo miradi minane iko Halmashauri ya Sengerema na miradi sita Halmashauri ya Buchosa.
Shamra shamra za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Sengerema.
Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kivuko cha MV. Mwanza kuelekea wilayani Sengerema kwa ajili ya mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo.
Vijana wa Skauti wilayani Sengerema wakiwa timamu kabisa kwa ajili ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Kaimu Mkuu wa Wilaya Misungwi, Petter Michael (kulia), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kaimu Mkuu wa Wilaya Sengerema, Joseph Kapunda (kushoto) Mwenge huo kwa ajili ya kuanza mbio zake wilayani humo.
Kaimu Mkuu wa Wilaya Sengerema, Joseph Kapunda (kushoto) akila kiapo cha kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru ukiingia rasmi wilayani Sengerema ukitokea wilayani Misungwi.
Kaimu Mkuu wa Wilaya Sengerema, Joseph Kapunda akiupokea Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili wilayani humo.
Viongozi mbalimbali wilayani Sengerema wakiulaki Mwenge wa Uhuru.
Viongozi mbalimbali wilayani Sengerema wakiulaki Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Willium Ngelema akiulaki Mwenge wa Uhuru.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Sengerema, Yanga Makaga akiulaki Mwenge wa Uhuru.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.