LIVE STREAM ADS

Header Ads

Miradi ya zaidi ya shilingi Bilioni 15 kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenge wa Uhuru 2019 umeanza kutimua mbio zake mkoani Mwanza ambapo utatembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Serikali na wadau binafsi yenye thamani ya shilingi bilioni 15.913 ambapo hadi tamati yake utakimbizwa kilomita 855.11 nchi kavu na majini notiko maili 72.

Mapokezi ya Mwenge huo yalifanyika jana Mei 14, 2019 katika uwanja wa Kijiji cha Mwawile kilichopo Kata ya Nhundulu wilayani Misungwi, ukitokea mkoani Shinyanga ambapo ulipokelewa na Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.

Ukiwa katika Wilaya Misungwi, Mwenge wa Uhuru chini ya Kiongozi wake kitaifa Mzee Mkongea Ali ulifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuweka jiwe la msingi mradi wa kuchakata na kufungasha nafaka Mwawile, kufungua nyumba ya waalimu (six in one) katika Shule ya Sekondari Isakamawe, kufungua jengo la kitengo cha Bima ya afya NHIF katika Hospitali ya Wilaya Misungwi, kuzindua klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya Msingi Misungwi, kuzindua mradi wa kutengeneza mikanda ya Gypsum Usagara pamoja na kukagua uendelevu wa mradi wa gesi ya majumbani wa Mwanza Gaz uliopo pia Usagara.

Aidha Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ali aligoma kuzindua mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya bomba katika Kata ya Ibinza pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya Misungwi-Mondo yenye urefu wa kilomita 23 inayojengwa kwa kiwango cha morani baada ya kukosekana baadhi ya taarifa muhimu za miradi hiyo.

Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendelea mkoani Mwanza hadi Mei 22, 2019 utakapokabidhiwa katika Mkoa jirani wa Simiyu, ukiwa na ujumbe usemayo “Maji ni Haki ya Kila Mtu, Tutunze Vyanzo vyake na Tukumbuke kushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwitio Chanya”.
Katibu Tawala mkoani Mwanza, Christopher Kadio akipokea Mwenge wa uhuru ulipowasili wilayani Misungwi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mwanza, Dkt. Antony Diallo akishika mwenge huo baada ya mapokezi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka mkoani Mwanza, Jamal Babu akishika mwenge huo.
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalika akiwa na Mwenge huo.
Mkuu wa Wilaya Sengerema, Mwl. Emmanuel Kipole akishika mwenge huo baada ya kuwasili mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akiwa na Mwenge huo.
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Peter Niboye akiwa ameshika Mwenge huo.
Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philimon Sengati akiwa ameshika Mwenge huo.
Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili mkoani Mwanza.
Katibu Tawala mkoani Mwanza, Christopher Kadio (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi, Kisena Mabuba (kulia) Mwenge huo kwa ajili ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Misungwi kwa ajili ya kuanza mbio zake wilayani huo.
Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi, Kisena Mabuba (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala mkoani Mwanza, Christopher Kadio (kushoto).
Katibu wa CCM Wilaya Misungwi, Ltifa Malimi akishika Mwenge wa Uhuru.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Misungwi, Daud Gambadu akiwa na Mwenge wa Uhuru.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza.
Katibu Tawala mkoani Mwanza, Christopher Kadio (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi, Kisena Mabuba (kulia) Mwenge huo kwa ajili ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Misungwi kwa ajili ya kuanza mbio zake wilayani huo.
Katibu Tawala mkoani Mwanza, Christopher Kadio (kushoto), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi, Kisena Mabuba (kulia).
Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi, Kisena Mabuba (kulia) akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili mkoani Mwanza..
Viongozi mbalimbali mkoani Mwanza, wakiukaribisha Mwenge wa Uhuru.
Tazama picha mbalimbali mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza.
SOMA>>> Habari mbalimbali za Mwenge wa Uhuru #PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.