LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yakutana na wadau wa mifuko mbadala na taka hatarishi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamuwa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba (katikati) akizungumza na wazalishaji wa mifuko mbadala ya plastiki (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini Dkt. Samuel Gwamaka. Kulia ni Dkt. Freddy Manyika ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira.

Pamojana mambo mengine, wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini. Haya yanajiri wakati Serikali imezuia matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Juni Mosi mwaka huu.
Na Lulu Mussa
Baadhi ya wazalishaji wa mifuko mbadala wakifuatilia mkutano huo.
Heneriko Batamuzi kutoka kampuni ya Kenwood Enterprise (T) Ltd akichangia mada katika kikao hicho cha wadau cha kupitia Rasimu ya Kanuni za kusimamia Taka Hatarishi hapa nchini. Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa rasimu ya Kanuni mpya za kusimamia Taka Hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na ukusanyaji, urejelezaji, uteketezaji na usafirishaji wake ndani na nje ya nchi.

No comments:

Powered by Blogger.