LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Magufuli atekeleza ahadi yake kwa wakazi wa Sengerema

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Kata ya Nyampande, Wilaya Sengerema mkoani Mwanza ya kuwaondolea adha ya upatikanaji wa maji imeanza kutekelezwa, baada ya Serikali kusaini mkataba na mkandarasi ili kutandaza mtandao wa maji ya bomba katika Kata hiyo.

Mkataba huo wa zaidi ya shilingi bilioni moja umesainiwa Mei 09, 2019 baina ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA) pamoja na mkandarasi kampuni ya HALEM ya jijini Dar es salaam mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM Construction ya jijini Dar es salaam, Mhandisi Happy Lebe (kushoto), wakisaini mkataba wa utekelezaji mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema. Aliyesimama upande wa kulia ni Mwanasheria wa MWAUWASA, Oscar Twakazi na kushoto ni Meneja Vifaa kampuni ya HALEM, Steven Malima.
Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM, Mhandisi Happy Lebe wakikabidhiana mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema baada ya pande zote mbili kuusaini.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.