LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi na wafanyabiashara watakiwa kusalimisha mifuko ya Plastiki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Halmashauri ya Jiji la Mwanza imewahimiza wananchi pamoja na wafanyabiashara kusalimisha mifuko ya plastiki baada ya zuio la matumizi ya mifuko hiyo kuanza kutumika ifikapo Juni Mosi, 2019 nchini Tanzania.

Afisa Mazingira wa Halmashauri hiyo, Lidya Nyeme ametoa rai hiyo leo Mei 27, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati iliyochukuliwa ili kufanikisha zuio la matumizi ya mifuko hiyo.

Itakumbukwa Aprili 09, 2019 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipiga marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki na kubainisha kwamba matumizi ya mifuko hiyo yatakoma Mei 31, 2019 ambapo kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Environmental Management Act),  Serikali imetunga kanuni za mwaka 2019 za kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.