LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ukikutwa na mifuko ya plastiki, adhabu yake ni hii hapa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
By Omari Kilwanda-Wakili
Kimsingi kuna Makosa Makuu Matano yaliyotajwa na kukatazwa ndani ya Sheria husika. Sheria hiyo Ndogo inajulikana kama The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019. Sheria hii Ndogo imetungwa kwa Mujibu wa Kifungu Na. 230 (2) (f) cha Sheria inayojihusisha na Usimamizi wa Mazingira (The Environmental Management Act, Cap. 191)

A: MAKOSA
Kwa mujibu wa Kifungu/Kanuni Na. 8 Cha Sheria ya Kuzuia Matumizi ya Mifuko ya Plastiki ambayo ni The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019 kuna Makosa Matano ambayo ni;

Kuzalisha na Kuagiza Mifuko ya Plastiki (Kifungu/Kanuni Na. 8 a );
Kusafirisha nje ya nchi Mifuko ya Plastiki (Kifungu/Kanuni Na. 8 b );
Kuhifadhi na Kusambaza Mifuko ya Plastiki,(Kifungu/Kanuni Na. 8 c )
Kuuza Mifuko ya Plastiki, (Kifungu/Kanuni Na. 8 d );
Kumiliki na Kutumia Mifuko ya Plastiki (Kifungu/Kanuni Na. 8 e )

B: Adhabu
Kwa kila kosa tajwa hapo juu, Sheria husika imetaja Adhabu yake. Hivyo basi kuna Adhabu aina tano kama ilivyo kwa Makosa husika. Kifungu/Kanuni Na. 8 cha Sheria tajwa hapo kilichotaja Makosa Matano ndicho hicho kimetaja Adhabu ya kila Kosa kama ifuatavyo;

1. Adhabu kwa Wazalishaji na Waagizaji
Kifungu/ Kanuni Na. 8 (a) cha Sheria tajwa hapo juu, kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;

Faini isiyopungua Milioni 20 na isiyozidi Billioni 1
Kifungo Kisichozidi Miaka Miwili au vyote Kifungo na Faini tajwa hapo juu.

2. Adhabu kwa Wasafirishaji kwenda nje ya nchi
Kifungu/Kanuni Na. 8 (b) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;

Faini isiyopungua Milioni 5 na isiyozidi Milioni 20,
Kifungo Kisichozidi Miaka 2
Au vyote Kifungo na Faini tajwa hapo juu.

3. Adhabu kwa Wanaohifadhi na Wasambazaji
Kifungu/Kanuni Na. 8 (c) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;

Faini isiyopungua Milioni 5 na isiyozidi Milioni 50
Kifungo Kisichozidi Miaka 2,
Au vyote Kifungo na Faini tajwa hapo juu.

4. Adhabu kwa Wauuzaji
Kifungu/Kanuni Na. 8 (d) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;

Faini isiyopungua Laki 1 na isiyozidi Laki 5,
Kifungo Kisichozidi Miezi 3
Au vyote Kifungo na Faini tajwa hapo juu.

5. Adhabu kwa Watumiaji na Wanaomiliki
Kifungu/Kanuni Na. 8 (e) cha Sheria tajwa hapo kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;

Faini isiyopungua Elfu 30 na isiyozidi Laki 2
Kifungo Kisichozidi Siku 7,
Au vyote Kifungo na Faini tajwa hapo.
SOMA>>> Wananchi na wafanyabiashara watakiwa kusalimisha mifuko ya Plastiki

No comments:

Powered by Blogger.