LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mama aomba wasamalia wema wamsaidie mwanaye gharama za matibabu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Happiness Stephen Makala, mkazi wa mtaa wa Busulwa Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga anaomba msaada wa matibabu kwa mtoto wake aitwaye Rogathe Cyprian Makala mwenye umri wa miaka 18 ambaye anayesumbuliwa na ugonjwa wa ngozi kwa muda wa miaka 16 sasa.

Anasema amehanghaika katika hospitali mbalimbali hapa nchini lakini siku moja alikutana na Daktari Bingwa kutoka Apolo India katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ndipo akampima na kumgundua kuwa homoni zake ziko kwenye njia ya mkojo hivyo anatakiwa apatiwe matibabu ndani ya miezi tisa kwa kupatiwa dawa kutoka India ambapo kila mwezi inatakiwa shilingi 504,000 ambapo kwa miezi hiyo tisa ni sawa na shilingi milioni 4.5 (4,536,000).

Kwa mujibu wa Daktari huyo, binti huyo akifikisha umri wa miaka 20 ugonjwa huo wa ngozi utaweza kugeuka na kuwa kansa, na ataweza pia kuwa anazaa watoto wenye kisukari, na kichwa kikubwa na hata kuambukiza watu wengine kwa njia ya kuchangia choo.

Daktari huyo huwa anakuja kila baada ya mwezi hapa mkoani Shinyanga ambapo dozi ya dawa hiyo anatakiwa aanze Juni 2 mwaka huu ambapo itakuja na daktari huyo.

Mama wa binti huyo anasema yeye hana uwezo wa kumtibu binti yake, mume wake alishafariki kwenye ajali mwaka (2007) ambaye alikuwa Mhasibu wa shirika la umeme TANESCO mkoani Shinyanga.

Anasema mwanae huwa halali usiku kucha anashinda anajikuna tu na hata wakati wa jua kali huku vipele vikimtoka mwili mzima, na anatarajia kujiunga na kidato cha tano kwani amefaulu kidato cha nne.

Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo:
Vodacom: 0764 206 669 ukitaka kutuma kwa M-Pesa jina Happines Makala
Halotel: 0626 845 953 jina Eliud Makala
Happines Stephen Makala (kushoto) akiwa na mtoto wake Rogathe Cyprian Makala (18) ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi.
Msichana Rogathe Cyprian Makala akionyesha namna ugonjwa huo wa ngozi unavyomsumbua na kutoka vipele mwili mzima.
Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia, awasiliane kwa namba zifuatazo;
Vodacom: 0764 206 669 ukitaka kutuma kwa M-Pesa jina litasoma Happines Makala
Halotel: 0626 845 953 jina litasoma Eliud Makala

No comments:

Powered by Blogger.