LIVE STREAM ADS

Header Ads

Michezo ya UMISSETA 2019 yang'oa nanga mkoani Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) 2019, yamefunguliwa rasmi mkoani Shinyanga ambapo wanafunzi wanatarajia kuonyesha vipaji vyao kwa kushiriki katika michezo mbalimbali.

Mashindano hayo yalifunguliwa jana Mei 27, 2019 na Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainabu Telack kwenye viwanja vya michezo vya CCM Kambarage Shinyanga Mjini na kuhudhuriwa na wanafunzi wa Shule za Sekondari kutoka Halmashauri sita za Mkoa huo na kusindikizwa na wadogo zao wa Shule za Msingi. 

Michezo ambayo itashindaniwa ni mpira wa miguu, mpira wa pete, kikapu, wavu, riadha, mpira wa meza, kucheza ngoma, pamoja na kuimba kwaya, ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu, ambapo washindi watakwenda kushindana kitaifa. 

Akifungua mashindano hayo, Telack aliwataka wanafunzi hao kudumisha nidhamu kwenye mashindano hayo hata wale ambao watachaguliwa kwenda Mtwara kushiriki kitaifa wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu. 

Alisema michezo ni afya, humjenga mtoto kiakili,kinidhamu, kuibua vipaji na hivyo kusikitishwa na shule binafsi ambazo zimezuia wanafunzi wao kushiriki kwenye michezo hiyo na kuwataka waiche tabia hiyo mara moja, ikiwa huko ni kumnyima mtoto kuonyesha kipaji chake na kuweza kupata ajira hapo baadae. 

"Kuna taarifa tunazo eti baadhi ya shule binafsi zimezuia wanafunzi wao kutoshiriki michezo hii ya UMISSETA, ni jambo la ajabu sana, mfano baba yake na Mbwana Samatta angekuwa wakimzuai mtoto wake kushiriki kwenye michezo leo asingekuwa mchezaji wa kimataifa, hebu waruhusuni watoto wenu waonyeshe vipaji vyao kwani michezo ni ajira pia" alisema Telack. 

"Na nyiye wanafunzi ambao mnashiriki michezo hii ya UMMISSETA naombeni muonyeshe vipaji vyenu ambavyo mmepewa na Mungu, pamoja na kudumisha nidhamu ya hali ya juu hata huko mtakapokwenda Mtwara na siyo kwenda kuendekeza mapenzi, nataka muje na makombe hapa ya ushindi likiwEmo la nidhamu" aliongeza. 

Pia aliziagiza halmshauri zote za mkoani humo kutenga bajeti ya kila mwaka wa fedha shilingi Milioni mbili kwa ajili ya kufanikisha michezo hiyo ya UMISSETA licha ya kupata fedha zingine kutoka wahisani ili kuwa rahisishia maisha wanafunzi wakaokuwa kambini. 

Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa Shinyanga, Mohamed Kahundi akisoma risala ya ufunguzi wa michezo hiyo ya UMMISSETA, alisema changamo ambayo wanakabiliana nayo kuendesha mashindano hayo hadi ngazi ya taifa ni ukata wa fedha na hivyo kuomba wahisani waendelee kujitokeza kufadhili michezo hiyo.

Alisema kwa mwaka jana 2018 Mkoa Shinyanga ulifanikiwa kupeleka timu kwenye mashindano ya kitaifa, lakini haukufanya vizuri kwani ulishika nafasi ya 20 kati ya 28 sababu ya maandalizi kuwa mabaya kutokana na upungufu wa rasilimali fedha ambapo hata baadhi ya timu zilishindwa kuzipeleka kushiriki kwenye mashindano hayo. 

Kauli mbiu ya UMISSETA 2019 ni "michezo na sanaa kwa elimu bora na ajira".
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack akizungumza kwenye ufunguzi wa michezo ya UMISSETA 2019 mkoani humo. Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohamed Kahundi akisoma risala kwenye ufunguzi wa michezo hiyo. Mkuu wa Wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko akitoa salamu zake na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack kufungua michezo ya UMISSETA 2019 mkoani humo. Awali wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye ufunguzi wa michezo hiyo. Wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye ufunguzi huo.

No comments:

Powered by Blogger.