LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko azindua Soko Kuu la Madini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefanya uzinduzi wa Soko Kuu la Madini Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kutumia soko hilo kuuzia madini yao na kuachana na tabia ya utoroshaji wa madini.

Uzinduzi wa soko hilo unganishi Kanda ya Ziwa umefanyika leo Mei 08, 2019 katika jengo la Rock City Mall ambapo Biteko amebainisha kwamba uanzishwaji wa masoko ya madini nchini umesaidia ongezeko la kiwango cha uuzaji madini tofauti na hapo awali ambapo yalikuwa yakiuzwa kiholela na hivyo kuikosesha Serikali mapato.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akitoa salamu za tume kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya hali ya uanzishwaji masoko ya madini nchini ambapo amebainisha kwamba zaidi ya mikoa 10 tayari imeanzisha masoko hayo.
Mfanyabiashara wa madini, Kakono Kaniki akitoa salamu kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza.
Tazama BMG Online TV hapa chini
Mongella ajivunia Soko Kuu la Madini Mwanza "tunataka nchi ifaidike"

No comments:

Powered by Blogger.