Header Ads

Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika akutana na wabunge wapya wa bunge hilo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Kadama Malunde – Johannesburg, Afrika Kusini
Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele jana amekutana na wabunge wapya wa Bunge la Afrika wataoapishwa siku ya Jumatatu Mei 6,2019 wakati wa mkutano wa pili wa Bunge la Tano la Bunge la Afrika jijini Johannesburg Afrika kusini.

Mkutano huo wa kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Bunge la Afrika ikiwemo kuwaeleza historia na jinsi bunge hilo linavyofanya kazi umefanyika katika ukumbi mdogo wa makao makuu ya Bunge la Afrika uliopo Midrand, jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Masele ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini nchini Tanzania, aliwapongeza hao wabunge 26 kutoka nchi tano zikiwemo Eswatini, Msumbiji, Uganda, Zambia na Algeria kwa kuchaguliwa kuwakilisha katika Bunge la Afrika.

Kikao cha pili cha kawaida cha Bunge la Tano la Afrika kinatarajiwa kuanza siku ya Jumatatu Mei 6,2019 ambapo wabunge zaidi ya 250 watajadiliana juu ya kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu “Mwaka wa Wakimbizi na Watu Waliopotea” na suluhisho la kudumu juu ya tatizo la wakimbizi barani Afrika.

Mijadala mingine itahusu taarifa juu ya amani na usalama katika bara ikiwa ni pamoja na maendeleo ya hivi karibuni na hali ya kisiasa Libya, Sudan, Algeria na mchakato wa amani nchini Sudan Kusini. 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele akizungumza wakati wa mkutano na wabunge wapya wa Bunge la Afrika uliofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge la Afrika, Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele akiwakaribisha wabunge wapya wa Bunge la Afrika.
Sehemu ya wabunge hao wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele akielezea jinsi Bunge la Afrika linavyofanya kazi.
Sehemu ya wabunge hao wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele na wabunge wapya wa Bunge la Afrika.
Picha ya pamoja,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele na wabunge wapya wa Bunge la Afrika.

No comments:

Powered by Blogger.