LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyakazi wa Nyumbani Mwanza wasisitiza maslahi yao kuzingatiwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Nyumbani jijini Mwanza, Anna Flora Livine akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani Duniani yaliyofanyika viunga vya Kishimba jumapili Juni 16, 2019.

Mwenyekiti huo alitumia fursa hiyo kuwahimiza waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani kuzingatia maslahi ya wafanyakazi wao ikiwemo kuwalipa stahiki zao kwa wakati na kwa mujibu wa sheria ambapo kima cha chini ni shilingi 40,000 kwa mwezi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mfanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza, Makisensia Antony akizungumzia changamoto zinazowakabili wakati wa maadhimisho hayo ambapo alisema ni pamoja na wafanyakazi kuchelewa kulala huku wakiamka mapema na hivyo kukosa muda wa kupumzika tofauti na sheria za ajira.
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Davis Justine akitozungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alihimiza waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani kuzingatia haki na maslahi ya wafanyakazi wao kwa mujibu wa sheria.
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Tazama BMG Online TV haoa chini

No comments:

Powered by Blogger.