LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi wa Umma watakiwa kuzingatia Maadili ya Utumishi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, BMG
Viongozi wa Serikali na taasisi za umma wametakiwa kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni na maadili ili kuepuka migongano inayoweza kujitokeza.

Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari kwenye semina ya viongozi wa taasisi za umma mkoani Mwanza.

Jaji Mstaafu Nsekela alisema viongozi kutokuwa na maadili pamoja kuwa na migongano wa kimaslahi kunaweza kuwafanya kuingia kwenye kosa la jinai na matokeo yake ni kufungwa.

Hali halisi nchini inajionyesha kuwa ukiukwaji wa maadili na migongano ya maslahi inayowahusisha viongozi kwenye taasisi mbalimbali za umma ni tatizo kubwa.

"Kumekuwepo na viongozi ambao wanaamua mambo kwa maslahi binafsi bila kujali nchi na hivyo kupelekea uwepo wa mgongano wa kimaslahi na kutofuata maadili" alisema Jaji Mstaafu Nsekela.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alisema viongozi wanaoongoza taasisi za umma wanapaswa kuendeleea kujenga nchi kwa kuzingatia uadilifu na uminifu ili watumishi walio chini yao wajifunze kutoka kwao.

"Uadilifu ni kigezo kimojawapo katika uongozi bora, hivyo kila kiongozi wa umma ana wajibu wa kuuzingatia," alisisitiza Mongella.

Naye Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Phillis Nyimbi aliyekuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria semina hiyo alisema semina hiyo itawasaidia kupata elimu ambayo wataitumia kutimiza vyema majukumu yao huku wakiwaelimisha watendaji wengine ili watimize majukumu yao kwa kuzingatia maadili.
Picha ya pamoja, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella na watendaji mbalimbali.
#VideoCredi @GsengoTV

No comments:

Powered by Blogger.