LIVE STREAM ADS

Header Ads

The Desk and Chair Foundation yakabidhi miundombinu ya Intaneti kwa MPC

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Taasisi ya "The Desk & Chair Foundation", Sibtain Meghji (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko (kushoto) kifaa cha kusambaza mawasiliano ya mtandao wa Intaneti (Router) pamoja na nyaya za umeme (Cable) ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za chama hicho katika kutimiza vyema majukumu yake ya kihabari katika jamii.

BMG Habari
Taasisi ya “The Desk & Chair Foundaton” ya jijini Mwanza imeunga mkono juhudi za Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club-MPC) kwa kukabidhi miundombinu ya Intaneti.

Mwenyekiti  wa taasisi hiyo, Sibtain Meghjee amemkabidhi Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko vifaa hivyo na kuahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na klabu hiyo katika kuchochea maendeleo ya Mkoa Mwanza.

Baada ya kupokea vifaa hivyo, Soko amesema uwepo wa miundombinu ya Intaneti ya uhakika kwa waandishi wa habari ni nyezo muhimu katika kutekeleza majukumu yao huku akiishukuru taasisi ya “The Desk & Chair Foundation” kwa mchango wake katika kuimarisha shughuli za waandishi wa habari.

Katika hatua nyingine, Edwin Soko ameongeza kuwa MPC itaendelea kufanya kazi na taasisi ya The Desk & chair pamoja na wadau mbalimbali wa Mkoa Mwanza pamoja na Serikali ya awamu ya tano na kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Mwanza.

“Uwezo wa miundombinu utasaidia waandishi wa habari kutuma habari zao na kupokea taarifa muhimu na pia kuhudhuria mikutano kwa njia ya mtandao” amesisitiza Soko.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni kipanga njia cha Intaneti kimoja (Router), waya za kuunganishia kifaa hicho, waya za umeme pamoja na vifushi vya intanenti ambapo hatua hii imekuja baada ya MPC kupata uongozi mpya Juni 01, 2019 ambao umeanza kujenga mahusiano mema na wadau wa habari ili kujenga mahusiano mazuri.
Kifaa hicho (Router) kutoka kampuni ya mawasiliano Tanzania (TTCL) kina uwezo wa kuunganisha kompyuta 30 kwa wakati mmoja hivyo kitasaidia wanachama wa MPC kupata huduma ya intaneti kwa uhakika huku pia wasio wanachama wakichangia gharama kidogo za uendeshaji.

No comments:

Powered by Blogger.