LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tamasha la Bulabo 2019 larindima uwanja wa Kisesa wilayani Magu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Tamasha la jadi, mila na desturi za kabila la Wasukuma (Bulabo) 2019 linaendelea kurindima katika uwanja wa Kisesa Wilaya Magu mkoani Mwanza kuanzia jumapili iliyopita Juni 23, 2019 hadi jumapili ijayo Juni 30, 2019.

Vikundi vya ngoma kutoka maeneo mbalimbali ya uskumani ikiwemo Mwanza, Shinyanga na Geita vinaendelea kuchuana vikali kwenye tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka kusherehekea sikukuu za mavuno huku likienda sambamba na ibada ya Ekaristi Takatifu (Corpus Christ- Mwili na Damu ya Yesu) ya Kanisa Katoliki.

Ufunguzi rasmi wa tamasha hilo mwaka huu ulifanyika jumatatu Juni 24, 2019 mgeni rasmi akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangalla huku viongozi wa Serikali na makabila kutoka mikoa mbalimbali nchini wakialikwa kushuhudia tamasha hilo ambalo kila mwaka huwa la kuvutia sambamba na ushindani mkali wa ngoma za kabila la wasukuma.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philemon Sengati akizungumza kwenye siku ya kwanza ya tamasha la Bulabo 2019.
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Magu, Lutengano Mwalwiba akitoa salamu zake kwenye tamasha hilo.
Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Magu, Hilal Elisha akisalimia siku ya kwanzaa ya tamasha la Bulabo 2019.
Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga akitoa salamu zake kwenye tamasha hilo.
Mratibu Mkuu wa tamasha la Bulabo ambaye pia ni Mtemi Mteule wa Nela Kwimba, John Shibuda siku ya kwanza ya tamasha hilo 2019.
Makamu Mwenyekiti wa tamasha la Bulabo 2019, Mama Hellen Bogohe akitoa salamu kwa niaba ya viongozi wengine wa kamati.
Viongozi mbalimbali wa Usukumani akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Watemi wa Usukumani, Mtemi Itale Charles Balele (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Watemi wa Usukumani, Mtemi Nyamilonda III Aron Mikomangwa (katikati).
Watemi kutoka makabila mbalimbali Tanzania wakishuhudia tamasha la Bulabo 2019.
Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Watemi wa Usukumaji, Mtemi Itale Charles Balele (kushoto) pamoja na Mtemi kutoka mkoani Mbeya (kulia).
Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watemi mbalimbali.
Tazama BMG Online TV hapa chini
Tamasha la Bulabo lazinduliwa kwa kishindo mkoani Mwanza
#Amaizing Tamasha la Bulabo #Usukumani Mwanza
Zifahamu sehemu kuu tano katika Makumbusho ya Wasukuma Bujora

No comments:

Powered by Blogger.