LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wazee wilayani Tarime wasisitiza kuachana na Ukeketaji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mmoja wa wazee wa kimila katika Wilaya Tarime mkoani Mara (kushoto) akieleza msimamo wa wazee wengine kutoka koo 12 za kabila la Wakurya wa kuachana na suala la ukeketaji wilayani humo huku akisisitiza elimu iendelee kutolewa katika jamii ili kutokomeza ukeketaji kwa wasichana.

Ni katika kikao kazi cha kutathimini utekelezaji wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wilayani Tarime awamu ya kwanza iliyokuwa inatekelezwa na Halmashauri ya Wilaya Tarime kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Tarime, James Gavana (kushoto) akikabidhi cheti kwa mmoja wa wazee wa kimila wilayani humo baada ya kushiriki vyema kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto awamu ya kwanza.
Viongozi mbalimbali wilayani Tarime wakiwemo Madiniwa, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo na waalimu walioshiriki vyema kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto awamu ya kwanza wilayani Tarime walipewa vyeti vya pongezi kutambua mchango wao.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Tarime, Ochieng Wayoga (kulia) akipokea cheti cha pongezi kutambua mchango wake katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wilayani humo.
Kata zilizofanya vizuri kwenye kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wilayani Tarime awamu ya kwanza ni Muriba, Ganyange, Bumera na Binagi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Tarime, James Gavana akizungumza kwenye hafla hiyo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Tarime, Ochieng Wayoga akizungumza kwenye kikao kazi cha kutathimini utekelezaji wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wilayani humo kilichoambatana na uzinduzi wa kampeni hiyo awamu ya pili.
Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia wilayani Tarime wakiwemo wazee wa kimila wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Mwakilishi wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/ Rorya, Nshashi Bulube akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Wazee wa kabila wa Wakurya wakifuatilia kikao kazi hicho.
Wazee wa kimila wa kabila la Wakurya wakifuatilia kikao hicho.
Hii ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) hadi kufikia mwaka 2022.
Wadau wa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wilayani Tarime wakifuatilia kikao kazi hicho.
Baada ya tathmini ya kampeni ya awamu ya kwanza, awamu ya pili ya kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ilizinduliwa wilayani Tarime.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.