LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri Ulega "Sekta ya Uvuvi inahitaji wawekezaji wenye nia njema"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdullah Ulega akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Watumishi wa Taasisi wa Sekta ya Uvuvi nchini Somalia wanaopata mafunzo katika Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini (FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini (FETA) Yahya Mgawe akitoa taarifa namna wanavyotoa mafunzo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Watumishi wa Taasisi za Sekta ya Uvuvi nchini Somalia yanayofanyika katika cha Uvuvi Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Watumishi wa Taasisi za Sekta ya Uvuvi nchini Somalia wakiwa katika mafunzo katika Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchni (FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mwakilishi Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa Japan Kentaro Akutsu akitoa namna wanavyotoa ufadhili wa Mafunzo kwa Watumishi wa Sekta ya Uvuvi nchini Somalia ikiwa ni njia kuongeza ajira kwa vijana katika nchi hiyo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo yanayoendeshwa na Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini (FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdullah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Sekta ya Uvuvi nchini Somalia wanaopata mafunzo katika Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini(FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema katika kufikia uchumi wakati sekta ya Uvuvi ni sekta ambayo inahitaji wawekezaji makini ikiwemo kutumia wataalam wa Uvuvi wanaosoma vyuo vya ndani.

Ulega ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya watumishi 20 wa Taasisi za Sekta ya Uvuvi nchini walioletwa na Shirika la Kimataifa la Japani (JICA) katika Wakala ya vyuo Uvuvi (FETA) Mbegani Wilaya Bagamoyo mkoani Pwani.

Amesema sekta ya Uvuvi imekuwa na michango mingi bungeni katika kuona nchi inanufaika katika kuleta maendeleo kwa kufikisha dhamaira ya serikali ya kufukia uchumi wa kati. Ulega amesema kuwa kutokana na Wakala ya Vyuo vya Uvuvi kufanya vizuri ndio maana nchi nyingine wanakuja kujifunza nchini Tanznaia. 

Amewasaa wasomali wanaopata mafunzo wakayatumie katika kuwapa maendeleo nchini mwao. Amebainisha kwamba Wakala ya Vyuo vya Uvuvi kwa miaka miwili zaidi ya wageni 770 wamepata mafunzo katika Wakala hiyo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo Vya Uvuvi nchini (FETA), Yahaya Ibrahim Mgawe amesema kwa miaka hivi karibuni wameisha toa mafunzo kwa wanafunzi zaidi ya 700  kutoka nchi mbalimbali ambapo moja ya mafunzo ni utawala uvuvi, menejimenti na masoko.

Kwa upande wake Afsa Miradi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Veronika Balua amesema Japan imeamua kutoa mafunzo hayo kwa wasomali lengo nikutaka kutoa fursa ya ajilra kwa vijana ili kupunguza migogoro iliyopo ndani ya nchi yao na Mafunzo hayo yatachukua takribani wiki tano.

No comments:

Powered by Blogger.