LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zawadi nono baada ya Misungwi Sekondari/ Bwiru Girls kuondoa ziro

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2019, wanafunzi wa Shule ya wasichana Bwiru waliopata daraja la kwanza ni 78, daraja la pili 154, daraja la tatu 167, daraja la nne watano ambapo hakuna daraja sufuri.  Upande wa Misungwi Sekondari, wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni wanne, daraja la pili 33, daraja la tatu 24 ambapo hakuna daraja la nne na sufuri.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kikao kazi cha kuweka mikakati ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni pamoja na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa kike katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza. 

Kikao kazi hicho kilifanyika Ijumaa Julai 12, 2019 jijini Mwanza kikiambatana na zoezi la utoaji vyeti vya pongezi na kompyuta mpakato (laptops) 11 kwa viongozi mbalimbali waliosadia utekelezaji wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya Misungwi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI, Yassin Ally akionesha jedwali la matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2019 ambapo ufaulu umeongezeka katika Shule ya wasichana Bwiru pamoja na Misungwi Sekondari ikiwa ni matokeo ya kampeni iliyofanywa na shirika la KIVULINI kwa kushirikiana na waalimu pamoja na viongozi wa Halmashauri.
Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akizungumza baada ya zoezi la kukabidhi kompyuta mpakaTo kwa viongozi mbalimbali Ilemela na Misungwi.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga akitoa salamu zake kwenye kikao kazi hicho ambapo aliahidi ushirikiano wa kutoka katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
 Mkuu wa Shule ya Wasichana Bwiru, Mwl. Meckrida Shija akieleza namna juhudi za shirika la KIVULINI zilivyosaidia kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kike shuleni hapo.
Shirika la KIVULINI limekabidhi vyeti vya pongezi na kompyuta mpakato (laptops) 11 kwa viongozi mbalimbali waliosaidia utekelezaji wa kampeni ya kutokomeza mimba, ndoa za utotoni pamoja na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa kike katika Wilaya za Ilemela na Misungwi.

Zoezi hilo lilifanyika Ijumaa Julai 13, 2019 jijini Mwanza ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa KIVULINI, Yassin Ally alisema juhudi zilizofanywa na viongozi hao zimesaidia kupambana na mimba kwa wanafunzi wa kike na kuongeza ufaulu katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu katika Shule ya wasichana Bwiru pamoja na Misungwi Sekondari.

Katika matokeo hayo, wanafunzi wa Shule ya wasichana Bwiru waliopata daraja la kwanza ni 78, daraja la pili 154, daraja la tatu 167, daraja la nne watano ambapo hakuna daraja sufuri. Upande wa Misungwi Sekondari, wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni wanne, daraja la pili 33, daraja la tatu 24 ambapo hakuna daraja la nne na sufuri.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.