LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Neema Mgaya asaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Njombe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa Njombe, Neema Mgaya amekabidhi mifuko 380 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 5.5 (Tsh. 5,510,000) ili kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

Akikabidhi mifuko hiyo, mbunge Mgaya alisema itasaidia kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya, vyumba vya madarasa, mabweni, nyumba ya watoto yatima, nyumba za ibada pamoja na ofisi ya CCM mkoani Njombe.

Mbunge Mgaya alibainisha kwamba Kata zitakazonufaika na mifuko hiyo ya saruji ni pamoja na Kitisi, Lupembe, Ramadhani, Yakobi, Ihanga, Ulembwe, Igima, Udonja, Ilembula, Igwachanya na Mdandu.
#BMGHabari
Sehemu ya mifuko ya saruji iliyokabidhiwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa Njombe, Neema Mgaya (wa kwanza kulia) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

No comments:

Powered by Blogger.