LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko ashiriki mkutano na wadau wa Almasi mkoani Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Issa Mtuwa, Wizara ya Madini
Mkutano Mkuu mdogo wa wadau wa madini ya Almasi mkoani Shinganga umefanyika juzi Julai 04, 2019 chini ya Waziri wa Madini, Doto Biteko na kushuhudiwa mafanikio kadhaa kutoka kwa wadau hao. Miongoni mwa mafanikio hayo ni wadau kuipongeza serikali kuanzisha masoko ya madini, uelewa wa sheria ya madini kwenye baadhi ya vipengele, kutambua wajibu wa kulipa maduhuli ya serikali.

Mafanikio mengine ni kutolewa kwa nafasi za maafisa watatu kutoka serikali kwenda kusomea masuala ya uthamini wa madini na kuchangiwa kwa milioni thelathini kwa chama cha wachimbaji wadogo (FEMAT) na chama cha wachimbaji wadogo wanawake (TAHOMA) kila kimoja kikipewa milioni kumi na tano (15,000,000) vyote vikiahidiwa na mgodi wa Williamson Diamond Ltd na kukubali kwa mgodi huokushirikiana na serikali, polisi na viongozi wa FEMATA kupitia mipaka ya mgodi huo.

Biteko aliwasili kwenye mkutano huo majira ya saa sitamara baada ya kumaliza kikao cha ndanina uongozi wa Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Zainabu Telack. Mkutano huo ulihusisha wachimbaji wa madini ya Almasi, wanunuzi (Dealers) na wanunuzi wa kati (Blockers) mkutano ambao ulikuwa mithiri ya ule wa mkutano mkuu wa sekta ya madini uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 22-23/01/2019 na kuongozwa na Rais John Magufuli.

Kikao ambacho kilimridhisha sana Waziri biteko jinsi ya muitikio ya wadau wote walioshiriki. Akitumia staili ileile ya Rais Magufuli kwenye mkutano mkuu wa sekta ya madini uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 22-23/01/2019. Biteko aliendesha mkutano huo kwa kutoa fursa ya kumsikiliza kila mdau kueleza changamoto zilizopo akilenga kuzitatua na kuleta tija katika sekta ya madini hususani Almasi na kuona madini ya Almasi yakichangia pato la taifa.

Wakizungumza kwenye kikao hicho, Maige Nese alimwambia Waziri Biteko kuwa bado wachimbaji wadogo hawajawezeshwa vya kutosha ingawaje wao ndio chanzo cha mapato yanayokwenda serikalini kupitia leseni zao na mauzo ya madini kwa Blocker/Dealers, uchimbaji wao bado ni duni, vifa hawana. Ameiomba wizara isimamie sheria ipasavyo, na blockers asimame sehemu yake na dealers pia sehemu yake.

Masanja Meja ambae ni Blockers ameiomba wizara itoe elimu kwa wachimbaji wadogo, Blockers na Dealers ili kila mmoja aijue nafasi yake, ameongeza kuwa itakuwa vizuri pia kama TRA watakao kusanya mapato kupitia madini watokanae na Wizara ya madini kwani watakuwa na uelewa wa sekta huska na kupunguza migogoro huku akiwasilisha kilio kikubwa cha upungufu wa wataalam wa kuthaminisha madini ambapo kwa soko la Shinyanga lina mtaalam mmoja tuu.

Naye George Minoja Mgasha mchimbaji mdogo alianza kwa kuipongeza na kumshukuru waziri wa Madini kwa kuamua kwenda Shinyanga na kukutana na wadau hao na kufanya kikao cha pamoja. Mgasha aliwasilisha kilio chake kuhusu maeneo ya uchimbaji kuwa ni tatizo na kuongeza kuwa mashamba yao ya uchimbaji yanamilikuwa na migodi mikubwa. Anaiomba wizara iingilie kati. Alizitaja kata ambazo baadhi ya maeneo ya wachimbaji wadogo maeneo yao yamechukuliwa na Migodi mikubwa ni Kata ya Maganzo, Songwa, Mondo na Idokilo.

Baada ya michango mbalimbali kutoka kwa wadau wote Biteko aliwashukuru sana wadau, aliwahakikishia kuwa maoni yao yote yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi na kuanzia wiki ijayo wataona matokeo ya kikao hicho na hapo hapo alimuagiza Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga Joseph Kumburu wiki ijayo akae na kuongoza kikao cha wadau hao kuanisha yale yote yaliyoainishwa na ambayo yapo chini ya uwezo wake ayatatue na kuwasilisha taarifa wizarani.

Biteko alifurahishwa na uwepo wa mwekezaji wa mgodi wa Williamson DiamondsLtd, Richard Duffy aliyehudhuria kikao hicho kuitikia wito wa kuhudhuria kikao hicho akitokea Afrika Kusini. Alisema Williamson Diamonds Ltd ni mwekezaji wa kuigwa kwani anaheshimu na kufata taratibu zinazoelekezwa na serikali na ndio maana wamekubali kuuza sehemu ya madini ya Almasi (5%) ya wanayozalishwa kwenye soko la mkoa wa Shinyanga. Alimshukuru Richard Duffy kwa mchango wake kwa FEMATA na TAHOMA.Wenye jumla ya Tsh. Milioni Thelathini (30,000,000).

"Lazima niseme ukweli kampuni Williamson DiamondsLtd,chini ya uongozi wa Richard Duffy ni mwekezaji wa kuigwa, tunahitaji wawekezeji wanao heshimu serikali na sisi tunamheshimu kama mwekezaji, kila tulipokaa kutatua changamoto Williamson DiamondsLtdwamekuwa waungwana na mara zote wamekuwa wakikubaliana na mapendekezo ya serika". Alisema Biteko.

Awali kabla hajamkaribisha waziri kuzungumza na hadhara hiyo Katibu Mkuu wizara ya madini, aliwashukuru wachimbaji wa madini na wadau wote na kuwaambia kwamba mafanikio ya wizara ya madini katika kufikia lengo la ukusanyaji wapato uliovuka lengo la bilioni 310 hadi kufikia bilioni 335 linatokana na wao kufuata sheria na matakwa ya sheria ya madini kwa kila jambo linalo elekeza hivyo pongezi hizo sio za wizara bali ni zao.

Katika ziara hiyo Waziri Biteko aliambatana na Katibu Mkuu wizara ya madini Profesa Simon Msanjila, Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini Profesa Shukrani Manya, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Edwin Igenge, Mhasibu Mkuu Anthony Tarimo wote kutoka Wizara ya Madini.
Wadau mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Madini, Doto Biteko kwenye kikao hicho.
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akitoa mchango wake.

No comments:

Powered by Blogger.