LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ziara ya Mkuu wa Mkoa Mwanza katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye boti ya mwendokasi kuelekea kwenye kisiwa kidogo cha Ukara wilayani Ukerewe kwa ajili ya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo hii leo jumapili Julai 07, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shughuli ya ujenzi wa uzio, makaburi na mnara kwenye makaburi ya baadhi ya abiria waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV. Nyerere mwezi Septemba mwaka jana 2019 inaelekea ukingoni.
Sehemu ya makaburi ya baadhi ya abiria wa kivuko cha MV. Nyerere waliopoteza maisha baada ya kivuko hicho kuzama mwezi Septemba mwaka jana 2018.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali amekagua ujenzi wa uzio, mnara na makaburi ya pamoja ya baadhi ya abiria waliofariki kwenye ajali ya MV. Nyerere.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John  Mongella katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe hii.
Tenki la maji lililojengwa kwenye Kituo cha Afya Bwisya kisiwani Ukara.
Sehemu ya majengo yaliyojengwa kwenye Kituo cha Afya Bwisya kupitia sehemu ya fedha za maafa ya kivuko cha MV. Nyerere.
Mwonekano wa majengo mapya katika Kituo cha Afya Bwisya kilichojengwa na kukarabatiwa kwa hadhi ya Hospitali ya Wilaya.
Ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya Bwisya unaelezwa kufikia asilimia 95 hivyo matarajio ni kukamilika hivi karibuni.
Kukamilika kwa upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya kutasaidia wakazi wa Kisiwa cha Ukara kupata huduma za afya kituoni hapo na kuondokana na adha ya kufuata huduma za afya mjini Nansio Ukerewe ama jijini Mwanza.
Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alielekeza sehemu ya fedha za maafa ya kivuko cha MV. Nyerere itumike kujenga na kukarabati Kituo cha Afya Bwisya ambapo shilingi milioni 800 zimetumika kufanya shughuli hiyo kama inavyoonekana kwenye picha.
Upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya umefanywa na kampuni ya SUMA JKT kwa usimamizi wa karibu wa kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Mkuu wa Wilaya Ukerewe, Colnel Magembe anasema wakazi wa Kisiwa cha Ukara wanaomba Kituo cha Afya Bwisya kitakapokamilika kifunguliwe rasmi na Rais Dkt. John Magufuli
Shughuli ya ufunikaji masinki ikielekea ukingoni kituoni hapo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewapongeza vijana wa JKT walioshiriki kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Bwisya.
Pia Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alitembelea Shule ya Sekondari Nyamanga kisiwani Ukara kujionea maendeleo ya ukarabati wa vyumba vya madarasa pamoja na ujenzi wa majengo ya maabara.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyamanga ulianza mwaka 2014 lakini utekelezaji wake ukaishia njiani hadi mwaka huu Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alipofanikisha ufunguzi wa shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua ukarabati vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Nyamanga kisiwani Ukara.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kisiwani Ukara.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.