Header Ads

Mwanza watakiwa kuwa na vyoo bora ifikapo Septemba 30, 2019

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ameagiza hadi kufikia Septemba 30, 2019 kila Kaya katika Halmashauri zote kuhakikisha inakuwa na choo bora, hatua itakayosaidia kuondokana na magonjwa ya mlipuko yanayogharimu fedha nyingi kwa ajili ya matibabu.

Agizo hilo la Mongella lilitolewa jijini jana jumapili Julai 07, 2019 na Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyinbi kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Nyumba ni Choo inayoratibiwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikilenga kuhamasisha ujenzi na matumizi ya vyoo bora.

Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya Kaya elfu sita hazina vyoo kabisa mkoani Mwanza huku Kaya zenye vyoo bora zikiwa ni asilimia 61 ambapo Kaya zenye vyoo ingawa si bora zikiwa ni asilimia 39.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya Nyumba ni Choo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella. Uzinduzi huo ulifanyika jana kwenye viunga vya Rock Beach jijini Mwanza.
Mhamasishaji wa kampeni ya Nyumba ni Choo, Mrisho Mpoto akieleza madhumuni ya kampeni hiyo.
Kampeni ya nyumba ni choo inalenga kuhamasisha wananchi kujenga na kutumia vyoo bora.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (katikati) akipiga picha ya pamoja na kikundi cha hamasa kwa kutumia nyoka kwenye kampeni ya nyumba ni choo.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba (katikati) akipiga picha ya pamoja na kikundi cha hamasa kwa kutumia nyoka kwenye kampeni ya nyumba ni choo.
Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha akipiga picha akiwa amemshika chatu.
Uzinduzi wa kampeni ya Nyumba ni Choo mkoani Mwanza ulitanguliwa na matembezi kutoka uwanja wa Nyamagana hadi katika viunga vya Rock Beach.
Vikundi mbalimbali vya hamasa vikionyesha burudani.
Burudani kwa njia ya sarakasi.
Kikundi cha hamasa kikitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi wakiwatuza watumbuizaji kwenye uzinduzi huo.
Sehemu ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya Nyumba ni Choo mkoani Mwanza.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.