LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkutano mkubwa wa Injili kutikisa jijini Mwanza "unakosaje sasa"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kanisa la kimataifa Lumala Mpya (Lumala Mpya International Church- LMIC) lililopo jirani na Soko Kuu la Sabasaba Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, limeandaa mkutano mkubwa wa injili utakaoanza Jumanne Julai 30, 2019 hadi Jumapili Agosti 04, 2019 katika uwanja wa Shule ya Msingi Sabasaba jirani na Kona ya Kiseke barabara ya Airport.

Wahubiri wa kimataifa wanatarajiwa kuhudumu kwenye mkutano huo wakiongozwa na Wachungaji wenyeji Dkt. Daniel Moses Kulola na Mercy Daniel Kulola pamoja na Wainjilisti Code Persell na Jeff Symons kutoka Marekani.

Tayari waimbaji mbalimbali wakiwemo Masanja Mkandamizaji, Ambwene Mwasongwe,  Martha Baraka, Daniel Cosmas pamoja na wenyeji Havillah Gospel Choir, Revival Choir, New Salvation Choir, Cecilia Emmanuel, Esther Nyanda, Joshua Samwel, Happy Emmanuel pamoja na Mariam Samwel wamethibitisha kuhudumu kwenye mkutano huo.

Watu wote mnakaribishwa kwenye mkutano huo mkubwa wa jijini Mwanza ambapo wagonjwa na wenye mahitaji mbalimbali wataombewa bure kwa jina la Yesu. Kwa msaada zaidi piga simu nambari 0767 74 90 40.
Mchungaji mwenyeji Dkt. Daniel Moses Kulola atahudumu kwenye mkutano huo.
Mchungaji mwenyeji Mercy Daniel Kulola atakuwepo.
Mwimbaji Masanja Mkandamizaji tayari kathibitisha kuwepo.
Mwimbaji Ambwene Mwasongwe atahudumu kwenye mkutano huo.
Mwimbaji Martha Baraka pia atakuwepo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.