Header Ads

Bashe aombwa kusaidia uendelezaji Kituo cha Utafiti wa Kilimo wilayani Chato

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kupitia wizara hiyo ameombwa kusaidia uendelezaji wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Bwanga kilichopo Wilaya Chato mkoani Geita ili kisaidie kuongeza tija kwa wakulima.

Mkuu wa Wilaya Chato, Mtemi Msafiri alitoa ombi hilo jana Agosti 03, 2019 wakati akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel kwenye ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.

Katika ufunguzi huo, salamu za Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ziliwasilishwa na Mkuu wa Wilaya Sengerema, Mwl. Emmanuel Kipole aliyebainisha kwamba uzalishaji umeendelea kuongezeka kwenye mazao ya kilimo hatua ambayo itakasaidia kufikiwa kwa uchumi wa viwanda.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.