Header Ads

MISA Tanzania yachukua hatua kuelekea chaguzi zijazo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Washiriki wa mafunzo kwa viongozi (wahariri, mameneja na wakurugenzi) wa vyombo mbalimbali vya habari Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja. Mafunzo hayo ya siku tano kuanzia jumatatu Julai 22, 2019 yanafanyika jijini Mwanza, yakiandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa kushirikiana na ile ya IREX kutoka Marekani pamoja na Ubalozi wa Marekani.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mkufunzi kutoka nchini Ufaransa, Linda Hervieux akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki Joas Kaijage kutoka Kagera Community Radio akiwasilisha kazi za makundi kwa niaba ya wenzake.
Mkuu wa Vipindi Star TV (Sahara Media Group), Moses Buhilya akiwasilisha kazi za makundi kwa niaba ya wenzake.
Mhariri wa Kanda ya Arusha, Mussa Juma kutoka kampuni ya Mwananchi Communications Limited akitoa mrejesho kwa niaba ya washiriki wenzake kwenye mafunzo hayo.
Farouq Karim kutoka ITV Zanzibar akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mhariri kutoka kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Peter Saramba akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Mkinga, Dastan Kitandula akitoa salamu zake kwa washiriki wa mafunzo hayo. Mbunge huyo ni mmoja wa wabunge marafiki wa MISA Tanzania.
Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo viongozi wa viongozi wa vyombo vya habari Tanzania kusimamia weledi kazini.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.