Header Ads

Viongozi wa vyombo vya habari Tanzania wapigwa msasa kusimamia weledi kazini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akifafanua jambo kwenye mafunzo kwa viongozi (wahariri na mameneja) wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mtaalam Mkufunzi kutoka nchini Ufaransa, Linda Hervieux akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
 Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania, James Marenga akiwasilisha mada kuhusu sheria mbalimbali za habari kwenye mafunzo hayo. 
 Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa Wakili James Marenga.
 Mhariri kutoka kampuni ya Sahara Media Group (Star TV) ya jijini Mwanza, Leonard Mapuli akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mkuu wa Vipindi Star TV Mwanza (Sahara Media Group), Moses Buhilya (wa tatu kulia) akiongoza wanakikundi wenzake kufanya kazi za makundi kwenye mafunzi hayo.
 Baadhi ya washiriki Deogratius Nsokolo (kushoto) kutoka ITV Mkoa Kigoma pamoja na Veronica Natalis (kulia) kutoka DW Mkoa Arusha wakijadiliana jambo kwenye mafunzo hayo.
 Japhet Sanga kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania (kulia) pamoja na Sarah Bushman kutoka taasisi ya IREX Marekani (kushoto) wakifuatilia mafunzo hayo.
 Washiriki wakitoa mrejesho wa kile walichojifunza kwenye mafunzo hayo.
 Mhariri kutoka Clouds Media Group, Joyce Shebe (kushoto) akitoa mrejesho wa kile alichojifunza kwenye mafunzo hayo mbele ya wenzake.
 Mkuu wa Kituo Msaidizi kutoma Redio Victoria FM iliyopo Msoma mkoani Mara akitoa mrejesho kuhusu alichojifunza kwenye mafunzo mafunzo hayo.
Mafunzo hayo ya siku tano yalianza Jumatatu Julai 22, 2019 hadi Ijumaa Julai 26, 2019 katika hotel ya Aden Palace Hotel jijini Mwanza, yakiandaliwa na taasisi ya MISA Tanzania kwa kushirikiana na ile ya IREX kutoka Marekani pamoja na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

Mada mbalimbali zinawasilishwa kwenye mafunzo hayo kwa viongozi wa vyombo vya habari nchini Tanzania ili kuwajengea uwezo wa kusimamia weledi kazini ikiwemo kuhakikisha habari linganifu hususani kipindi cha uchaguzi zinapewa kipaumbele.

Mada nyingine ni pamoja na jukumu la vyombo vya habari katika kukuza demokrasia, uandishi wa habari unaozingatia maadili, usalama wa waandishi wa habari mtandaoni, nafasi ya mwanamke katika vyombo vya habari na chaguzi mbalimbali pamoja na tahadhari wanazohitaji waandishi wa habari wakiwa kwenye mazingira hatarishi ya kazi. 

No comments:

Powered by Blogger.